Zinazobamba

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) laandaa vitabu vya uchambuzi elimu ya msingi, naye kassimu Majiliwa awataka walimu wa shule za msingi kuvitumia

https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQCeSysSXgANYmLFMRvadF7bMLZSONSVMPNlPUPJ3hTL0nNi0-j
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Shukuru Kawamba, picha na maktaba

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limeandaa vitabu vya uchambuzi wa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2013, ambapo imeeleza ubora na changamoto zinazoikabili shule.

Uchambuzi huo, umelinga kuamsha ari ya ufundishaji wa shule na kusaidia serikali kutatua changamoto kadhaa zinazoikabili shule katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN).

Vitabu hivyo vilizinduliwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye alisema vitabu hivyo vitasaidia kubainisha mapungufu na changamoto zilizowakumba wanafunzi wakati wa kufanya mitihani yao ya mwisho.

Alisema NECTA imefanya jambo nzuri kwa kuwa vitabu hivi vimebainisha ubora wa shule ya kwanza hadi ya mwisho, hivyo kila shule itatakiwa kujitahidi kuhakikisha inaondoka nafasi iliyopo na kufika nafasi za juu zaidi.

Alisema mpango wa serikali wa BRN kwa Necta umeanza kuonyesha mafanikio hasa kwa kuja na vitabu hivyo, ambapo wadau wa elimu wanatakiwa kuvitumia ili kuboresha elimu nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa aliwaagiza maofisa elimu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatumia vitabu hivyo.

Alisema vitabu hivyo vitawasaidia kuangalia wapi kuna upungufu na changamoto ili kuweza kuzifanyia kazi na zisijirudie tena katika matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne nchini.

Awali, Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde alisema vitabu hivyo vimechambua mitihani yote mitano waliyofanya mwaka jana lengo likiwa ni kupata uwanja mpana wa mafanikio.

Kwa mujibu wa Dk. Msonde alisema kila swali limeelezea na kufanyiwa tathimini ni wanafunzi wangapi walilifanya, wamelikosa na wamelipata.

Hivyo, Kaimu huyo alisema wasome vitabu hivyo kwa kuwa vimeeleza kwa nini wanafunzi wamekosa na kwa nini wengine wamelipata na watumie kwa ajili ya kufanya maboresho.

Hakuna maoni