sheikh ponda akwama tena mahakamani,
Sheikh Ponda Akwama
Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP), ameendelea kuweka pingamizi dhidi ya Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda akipinga maombi
yake ya kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, akidaiwa kufanya uchochezi
maeneo mbalimbali mkoani humo na kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu ya
Mei 9, mwaka jana ya kumtaka kuhubiri amani kwa jamii likiwa ni sharti
la kifungo cha mwaka mmoja nje.
Awali,
Sheikh Ponda aliomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro imfutie shtaka
hilo la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu, lakini Mahakama ya Hakimu
Mkazi Morogoro ilimkatalia, aliamua kuwasilisha maombi Mahakama Kuu
akiiomba ifanye marejeo ya uamuzi huo.
Hata hivyo, maombi hayo yalitupiliwa mbali Desemba 11,
mwaka jana baada ya DPP kumwekea pingamizi kuwa hati ya kiapo iliyokuwa
ikiunga mkono maombi yake, ilikuwa na kasoro za kisheria kwa kuwa
haikuwa ikitimiza matakwa ya Sheria ya Viapo kwa kutokuonyesha jina la
aliyeapa na tarehe.
Baada ya kutupiliwa mbali, Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro aliwasilisha tena maombi hayo.
mahakamani hapo baaada ya kufanya marekebisho ya kasoro hizo za kisheria.
Maombi
hayo mapya yalipangwa kusikilizwa jana na Jaji Augustine Mwarija,
lakini yalikwama baada ya DPP kuwasilisha tena pingamizi la awali
akiiomba mahakama iyatupilie mbali akidai kuwa yamewasilishwa kinyume na
kifungu cha 372 (2) Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni