JINSI ZITTO, MKUMBO WALIVYOJIBU MAPIGO,WADAI HATOKI MTU
Na Karoli Vinsent
MBUNGE wa kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe ameibuka na kujibu mapigo na kusema haondoki Chadema.
Hayo aliyasema leo jijini Dar
es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wahariri Zitto
alisema kwa sasa hanampango wa kuondoka chadema kama watu wanavyosema na kusema
kuwa yeye atakuwa mtu wa mwisho kuondoka
“Nawahakikishia siwezi
kuondoka chadema na kama kuondoka mimi
nitakuwa mtu wa mwisho kukihama chadema,siwezi nikahama Chadema akati
nimejiunga tangu na miaka 16 mimi nimepanda miti ya hiki chama mpaka leo
kimestawi harafu nikihame haitowezekana”alisema Kabwe

Kuhusu kufukuzwa uongozi wa
Chadema
Zitto Kabwe alisema mpaka sasa hajapata
barua kutoka kwa Viongozi wa Chama kuhusu kufukuzwa kwake katika uongozi na
kuongeze kuwa yeye anachosubilia ni barua hiyo
“Mimi nichosubili ni barua
kutoka kwa viongozi wa Chadema wananiambie wameniengua katika Uongozi na Sababu
waziweke hadharani,na mimi nitachukua hatua ya kukata rufaa sehemu
zengine”alisema zitto
Vilevile Kabwe alimtaka
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ambae pia ni Mbunge wa singida
Mashariki, atoe ushahidi kama Zitto kabwe
anahusika katika Ripoti hiyo ya siri,
Zitto aliongeza na kusema
Lissu amevunja kanuni za Chama katika kutoa hukumu hiyo
“Ukisoma vipengere mbalimbali
vya katiba ya Chadema inasema wazi kuhusu kumuengua kiongozi pamoja na
kumfukuza mwanachama,ni pamoja na kumpa mda wa kujitetea pamoja na kuonyesha
ushahidi wa kosa lenyewe lakini leo Chadema hawajafanya hivyo wametoa mahamuzi
ambayo yako nje ya Katiba ya chadema”alisema Kabwe
Kwa upande mwingine Zitto
Kabwe amefadhaishwa sana
hari ya kisiasa ndani ya chama cha Chadema na kusema kuwa hali hiyo haitasaida
kujenga chama bali ndio itakuwa inakishusha chama hicho
“Siasa za Majungu ndani ya
Chadema haita kisaidia Chama na hari hii Chadema inapitia katika sehemu ngumu
sana Chadema si chama Cha kwanza kupitia hali hii ni vyama vingi sana vinapitia
katika hali hii,na hali hii ni ishara tosha kabisa kuwa ni kukomaa kwa
Demokrasia na kikipa nguvu chama’”alisema kabwe
KUHUSU DK KITILA MKUMBO
KUENGULIWA NAFASI YA UONGOZI
Kwa upande wake kitila mkumbo
yeye alisema amefadhaishwa na maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu na kusema
hawajafuata haki
“mimi sijakubalina na
maamuzi
ya wajumbe kwani hawajafuhata haki katika maamuzi haya kwani katiba ya
chama
hiko wazi katika kuwaengua viongozi lakini leo chadema hawajafata
vipengere kama kumpa mwanachama au kiongozi kujitetea pamoja na
ushahidi wa kile anachokifanya na huo walaka ambao tunahukumiwa uko
sahihi”alisema Mkumbo
Vilevile kuhusu hoja ya
kukihama Chama Mkumbo alisema kwa sasa hatokiahama chama cha chadema na hataendeleo kupigania hati ya
watanzania na hatua chama hicho kinapitia ni hatua ya kukijenga chama na chama
chochote duniani cha kisiasa kinapita
sehemu hiyo
KUHUSU WALAKA WA SIRI KUHUSU MABADILIKO YA CHADEMA
Kuhusu
hoja
ya walaka mbunge Zitto Kabwe pamoja
na Mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu cha mrimani Dokta Kitila Mkumbo
wote
kwa pamoja waliunga mkono yale yalioandikwa ndani walaka huo na kuongeza
kuwa kama mtu anayependa mabadariko lazima haukubali walaka
huo
“Mimi sikuwaikusoma walaka
huo niliuona mala ya kwanza kwenye mkutano mkuu wa chama juzi na nilipousoma
nikaukubari walaka huo na kuvikubali vipengere vyote vilivyoandikwa katika
walaka huo”Alisema Zitto Kabwe
Kwa upnde wa Dk Mkumbo
alisema walaka huo umeandikwa mahasusi kwa ajiri ya kukijenga chama cha Chadema
“Walaka huu unaonyesha
taswira ya kukijenga chama chetu kukitoa
katika mfumo wa kidikteta na kukifanya kiwe chama cha nchi nzima”alesema Mkumbo
Katika hali ya kushangaza
Waandishi wa habari walimbana Dk Mkumbo hawataje watu waliohusika katika kuandaa
walaka huo lakini Dk huyo aligoma kuwataja wenzake na kusema kuwa kila mtu
ajitangaze mwenyewe kwa wakati wake
Mwandishi wa Blogs hii aliushuhudi
walaka huo ikiwa pamoja na kuusoma walaka huo huku walaka huo ukionyesha
udhaifu mkubwa katika Chama hicho cha siasa chadema na katika suala la uongozi
na kuonyesha chama hicho akina uwazi wa mapato na mtumizi ya pesa pamoja na
viongozi wa juu wachadema katika kuchezea katiba ya Chama hicho ili waendelee
kubaki daima
Taarifa
ya chamaAkitangaza uamuzi wa Kamati Kuu jana Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto, Dk Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walikuwa na mtandao wa kukiua chama hicho, huku wakitengeneza tuhuma za kuwachafua Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk Willbroad Slaa.
Alisema kuwa kamati kuu ilibaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
“Kikundi hicho vinara wake wapo wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne hatujamtambua kwa sasa yeye anatumia jina la M2” alisema Lissu.
Alisema wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu Dk Mkumbo alikiri kuwa mhusika mkuu wa mtandao huo ni Zitto, lakini Zitto alikana kuutambua waraka huo licha ya kueleza unamhusu kwa kuwa umetaja jina lake, kauli ambayo alidai Kamati Kuu haikutaka kuiamini.
Huku akieleza jinsi watu hao walivyokuwa wakiwasiliana na kupanga mikakati ya kuimaliza Chadema kwa siri chini ya ufadhili wa fedha kutoka kwa Zitto, Lissu alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa zamani alikuwa akitumiwa na Chama Tawala (CCM) kuimaliza Chadema.
“Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichanachana katiba ya chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba.
Alisema Kamati Kuu itakutana
kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya watuhumiwa hao
KUHUSU RIPOTI YA SIRI KUHUSU ZITTO KABWE
KWA
upande wa ripoti ilyosambazwa kwenye mitandao ya kijamiii kuhusu Zitto Kabwe
kushirikiana na Viongozi wa Juu wa Usalama wa Taifa katika kukihujuma Chadema Ripoto
hiyo iliyojulikana kama “Ripiti ya Siri kuhusu
Zitto Kabwe
Zitti Kabwe alisema yeye alipousoma walaka huo
aliwasiriana na viongozi wa chama na kuwauliza wao kama
wana utambua walaka huo na wao wakakanusha kile kilichoandikwa kwenye walaka huo
“Mimi nilipousoma ripoti hiyo
nikawasiliana na viongozi wachama na kutaka kuja kama wao wanahusika katiaka
ripoti hiyo ila wao kwa pamoja wakakanusha kama chama kinahusika kuuandaa
walaka huo na kusema ni hila zinazofanywa na CCM pamoja na jkushirikiana na
usalama wa Taifa”alisema Zitto Kabwe
Vilevile Zitto kabwe aliongeza na kusema kuwa kwa sasa
anatawachukulia hatua viongozi wote wa chadema waliohusika katiaka kusambaza
walaka huo,ikumbukwe mwandishi wa blog hii aliripoti kuwa walaka huo
unasambazwa kwenye blogs ya kiongozi wa Chadema na jina tumeliifadhi
KUHUSU POSHO
KUHUSU posho
Kabwe alisema apokei posho toka mwaka 2008 na anafanya hivyo ili kupinga posho
zinazotolewa bungeni kwenye vikao vyake pamoja na Shuguli za Kamati na
kufafanua kuwa posho hizo zingeenda kwasaidia wa mama wajane wanaojifungulia
vichakani kwa kukosa hospitari na zingeelekezwa kwenye kujenga shure.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Alimtuhumu mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Zitto alijibu kuwa tangu siku nyingi alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’ iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuihujumu Chadema.
Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.
Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo. Vyama vinavyopata ruzuku ya Serikali ni vile vyenye wabunge Chadema, CCM, UDP, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi.
MWISHO
Hakuna maoni
Chapisha Maoni