Zinazobamba

BREEKING NEWS , KAPUYA ADAIWA KUMBIA NCHI, ADAIWA KUKIMBILIA SWEDEN

 http://www.mjengwablog.com/images/101/JumaKapuya_85afa.jpg


Na Karoli Vinsent

SIKU moja baada ya binti anayedaiwa kubakwa na kutishiwa kuuawa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kufungua jalada polisi dhidi yake, inadaiwa mbunge huyo ametoweka nchini,FULLHABARI INATIRIRIKA NAYO.

Vyanzo mbalimbali vilivyo karibu na mbunge huyo, vinadai kuwa amesafiri juzi kwenda nchini Sweden kwa masuala ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini Sweden miezi miwili hadi mitatu.

Hata hivyo haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna taarifa safari hiyo imelenga kumtuliza na upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.
Wakati Profesa Kapuya anakimbilia nje ya nchi, tayari alishafunguliwa jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam juzi.


Mtoa taarifa wetu anasema muda mchache baada ya Kapuya kushindwa kumshawishi binti huyo asimfungulie kesi ya ubakaji, wala kuogopa vitisho vya kuuawa, au kupokea pesa kiasi chochote aondoke nchini, Kapuya mwenyewe alipanga safari ya dharura na kwenda nje ya nchi.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA alipofanya juhudi za kuwasiliana na ofisi ya Bunge kujua kama wana taarifa zozote za kuondoka kwa mbunge huyo kwenda nje ya nchi na kujua ni sababu zipi hasa zimempeleka huko, lakini simu ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ilikuwa inaita bila kupokelewa.
Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila naye hakupatikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakuujibu.
Hata hivyo,fullhabari  imedokezwa kuwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu ambayo Kapuya ni mjumbe wake haina safari ya Sweden.
Tangu gazeti moja hapa nchini lianze pamoja blogs hii lianze kuandika tuhuma hizi nzito, kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.
Harakati za kufungua jalada dhidi ya Kapuya zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.
Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.
Polisi wanena
Akizungumza na fullhabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake zitathibitika.

Alisema Jeshi la Polisi lina mtandao mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na kurejeshwa kwao.
“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana na hatufanyi kazi kinyume na taratibu zetu,” alisema.
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya huku akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.

Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Gazeti la Tanzania Daima limekuwa likiandika namba ya simu ya Prof. Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo, ingawa kuna vyombo vingine vya habari viliamua kuandika kwa mtazamo tofauti na kumtuhumu dada wa binti aliyebakwa kuwa ni mtu mzima na kuwa ana uhusiano na Kapuya na wana watoto.

Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.
Moja ya ujumbe wa vitisho unaodaiwa kutumwa na Kapuya kupitia simu hiyo unasomeka hivi: “Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe, sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo
“Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha tuone utalindwa milele maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana nasi.”


Pia simu hiyo iliwahi kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaosomeka hivi; “Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Sitta asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi? We unadhani nani atakaenifunga, ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone.”
Mbali na kutishia kumuua binti huyo na ndugu yake na mtu mwingine yeyote atakayejitokeza kumsaidia, gazeti hili limenasa baadhi ya mawasiliano ya simu za ujumbe mfupi wa kuhamisha fedha kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo ambaye mbunge huyo alikana kumfahamu na kwamba hajawahi kukutana naye.

Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo.
Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: U26UG365 Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000.
V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040.
R93NY448 Imethibitishwa Umepokea Tsh 505,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000.
Kutokana na mfululizo wa habari hiyo ambayo imekuwa ikichapishwa na gazeti hilo pamoja na blogs mbalimbali , Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake Yasin Memba, ametishia kuliburuza mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba

Hakuna maoni