Zinazobamba

ZITTO AJIBU MAPIGO, ASEMA HATOKI MTU CHADEMA HAPA, YEYE YUPO NA ATAZIDI KUWEPO,MWANASHERIA WA ZITTO AMPA SIKU 14 TUNDULISU >>>>

ALIYEKUWA naibu katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini, Mh. Zitto Kabwe hii leo amefunguka na kusema yeye chadema hatagong'oka na kwamba yeye atakuwa wa mwisho kutoka katika chama hicho tena kwa hiyari yake bila kushurutishwa na mtu,
ZITTO AKIWA SAMBAMBA NA DR MKUMBO AKISIKILIZA HOJA ZA WAANDISHI WA HABARI, MKUMBO NAYE AMESEMA BADO YUPOYUPO SANA CHADEMA,
Hayo ameyasema mapema hii leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Daresalaam, Zito amesema tuhuma ambazo zimeelekezwa kwake kwa kweli zimemfadhaisha sana na kumsumbua sana kimawazo huku tuhuma hizo zikiwa hazina ukweli wowote juu yake,

Kuhusu Walaka zito ameukana waraka huo kuwa hautambui nakwamba watu walioandaa waraka huo walikuwa na lengo la kuwagombanisha chama hicho kikuu ambacho kwa sasa wakati wa uchugazi unakaribia watu wanaamua kuwachanganya

Zito na Dr Mkumbo kupitia kwa wakili wao, wamemtaka mwanasheria mkuu wa chama cha chadema kuudhilishia ummma kwa namna gani watumiwa wametenda kosa kwa kuleta mbele ushahidi usio wa mashaka ili watuhumiwa nao wajibu kwa siku hizo kumi na nne ambazo wateja wake wamepewa,

Aidha mwanasheria kwa upande wake amesema kwa sasa wateja wake hawana haja ya kujibu hoja yoyote kwani tuhuma ambazo zimetaja kwa wametaja wake haziko kimaandishi na badala yake yamesikika kupita vyombo vya habari

Chama kina utaratibu wake wa kupashana habari, sio kwa kutumia vyombo vya habari ndio iwe taarifa rasmi kwa kwa wanachama wake, aliongeza Bwana Albart ambaye pia ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho



ZIITO ZUBERI KABWE AKIINGIA UKIMBINI TAYARI KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI, ZITO AMESEMA HATOKI CHADEMA, ATATOKA KWA HIARI YAKE












ZUBERI AKIMSALIMIA MMOJA WA WATU WALIOHUDHULIA KATIKA MKUTANO HUO, ALIYEKAA NI MAMAYAKE MBUNGE HUYO

Hakuna maoni