Zinazobamba

WANAWAKE ACT WAZALENDO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUWAKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA OKTOBA 29,2025.

Na Mwandishi wetu 

Dar es Salaam 

Ngome ya Wanawake ACT-Wazalendo imejiandaa kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kuomboleza kutokana na vifo,ulemavu wa kudumu waliopata baadhi ya Watanzania wakati wa ghasia zilizofanyika Oktoba 29,2025.

Hayo yamesemwa Februari 26,2026 na Mwenyekiti wa Ngome hiyo Janeth Rithe wakati akizungumza na Waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni Jijini Dar es salaam,nakubainisha kuwa siku hiyo wataisherehekea kwa kufanya maombilezo.

"Hatuwezi kufanya sherehe wakati mioyo ya watanzania inamwaga machozi kutokana na kupoteza  wapendwa wao na wengine kupata ulemavu wa kudumu mwezi Machi utakuwa ni mwezi wa Maombolezo." Amesema Rithe

"Nakuongeza kuwa " siku ya Machi 8,2026 tutafanya maombi na hitima pamoja na kutembelea wazee,watoto yatima,kufanya usafi vituo vya afya na kutoa msaada,kuchangia damu,kuzulu makaburi na kufanya mikutano mikubwa ya hadhara nchi nzima."

Aidha Mwenyekiti huyo wa Ngome ya Wanawake ACT  amesema kuwa kauli mbiu ya maombolezo hayo ni"Machozi ya mama ni deni la Taifa".

Amesema Ngome ya Wanawake ACT -Wazalendo ni sauti ya wale wasiojiweza kusema na hawawezi kunyamaza hadi pale haki itakapotendeka.

No comments