WAKULIMA IFAKARA WAPEWA MATUMANI KIBAO.
*Waahidiwa kupatiwa Trekta za Kilimo,kujengewa maghala ya kuhifadhia Chakula.
*Vijana kupewa power tiller kujiinua kiuchumi.
Pia ameahidi kuwapatia Vijana wenye umri kuanzia miaka 18 mashine aina ya power tiller kwa kila kijana ili aweze kujikwamua kiuchumi.
Ahadi hizo amezitoa Septemba 6,2025 wakati akihotubia Wananchi wa kata hiyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake,nakubainisha kuwa ahadi hizo atazitekeleza mara tu atakaposhika madaraka ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 29 Mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Morogoro ni Mkoa wenye utajiri mkubwa kutokana na kuwepo rasilimali Madini nyingi hivyo inasikitisha kuona Vijana wanakosa ajira huku Wananchi wakiishi maisha ya umasikini.
" Ndugu zangu kichagueni chama chenu,umati uliopo hapa ni ishara kuwa Oktoba 29 nitapata Ushindi wa kishindo, amesema Mwiru huku akishangiliwa na Wananchi waliojitokeza kumsikiliza.
Nakuongeza kuwa "nikiwa rais nitahakikisha kila kaya kumi zinapata trekta mbili kwa ajili ya kufanyia kilimo pamoja na kujenga maghala ya kuhifadhia mazao."
Pia amesema kuwa ataijenga stendi kuu ya kilosa kwa kiwango cha lami kwani kwa sasa miundo mbinu ya stendi hiyo ni mibovu na haina hadhi ya kuitwa stendi ya Wilaya ya Kilosa.
"Ndugu zangu tuna,hapa Morogoro tuna milima mingi ya mawe,nikiwa rais nitaleta mashine za kuponda mawe na kusaga kokoto(Crushers)ili tumwage lami na zenge kwenye barabara zote na hii stendi ya Wilaya ya kilosa"amesema.
Katibu Mkuu wa chama hicho Rashid Rai ameendelea kusisitisza kuondoa vyeo vya viongozi ambao hawana tija kwa wananchi.
Aidha amewaomba wanachi kutowalaumu Wabunge,Madiwani au Wenyeviti wa Serikali za mtaa ambao vyama vyao havijashika dola kwani shughuli za Maedeleo usimamiwa na chama kilichopo madarakani.
"Msiwalaumu wagombea wa Ubunge,udiwani na viongozi wa Serikali za mtaa,hawana uwezo wa kufanya chochote kama chama chake hakijachukua madaraka ya nchi hii, " amesema Rai
Nakuongeza"maana yake ni kwamba ili mambo yaende mnawajibika kubadilisha pale kwenye uongozi wa juu ili chama kikishika dola Wabunge,Madiwani na Wenyeviti wa Serikali ya mtaa wawe na nguvu ya kutekeleza shughuli za Maendeleo ".
No comments
Post a Comment