MWIRU ATETA NA WAFANYABIASHARA SOKO LA KISARAWE
*Asikitishwa na ubovu wa miundombinu ya soko hilo,atoa ahadi.
*Wafanyabiashara wampokea kwa shangwe,wamuahidi kura za ndio Oktoba 29,mwaka huu.
*Wasanii wanaovaa hereni kuchapwa viboko kumi na viwili.
*Mafisadi kutafunwa na mamba.
*Walimu,Polisi kicheko.
Na Mwandishi Wetu,Kisarawe Pwani.
(wajasiriamali )lililopo stendi ya Wilaya ya kisarawe Mkoani Pwani nakuzungunza nao.

Mheshimiwa Mwiru ametembelea soko hilo Septemba 10,2025, nakuahidi kuwa chama hicho kikishika dola Oktoba 29,Mwaka huu kitaondoa changamoto zote zilizopo kwenye soko hilo ili wafanyabiashara hao wafaidike na matunda ya Serikali yake.
" Soko hili lina miundombinu mibovu licha ya Serikali ya CCM kujinasibu kua imejenga masoko makubwa yenye hadhi ya wafanyabiashara wa kitanzania,nimejionea mwenyewe miundombinu ya soko lenu sio mizuri,nitafayia kazi siku nikiapishwa kua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema."amesema Mheshimiwa Mwiru.
Akizungumzia ahadi za Serikali yake Wilayani Kisarawe endapo atachaguliwa na Wananchi hao kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29,2025, Mhe.Mwiru amesema zipo changamoto nyingi zinatakiwa kutatuliwa ili kuwafanya wakazi wa Wilaya hiyo kunufaika na utajiri wa nchi yao.
*Wasanii wanaovaa hereni kuchapwa vipoko 12.
Amesema kuwa Serikali yake haitakua tayari kuona mwanamuziki yeyote amevaa hereni,kwani ni uvunjifu waaadili ya kitanzania,na mwanamuziki atakae vaa hereni atachapwa viboko kumi na viwili hadharani.
*Stendi ya Wilaya Kisarawe.
Amesema kuwa uwanja wa stendi hiyo una mawe kama misumari nakuwahakikishia Wananchi wa Wilaya ya Kisarawe wakiwemo waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda pamoja na mama na baba lishe kuondokana na vumbi kwenye biasharaza zao itakapo wekwa zege ndani ya miezi yake miwili ya kuingia Ikulu".
*Walimu kuishi kifalme.
Amesema kuwa walimu wanaishi kwa shida,mishahara duni,ambapo Mwalimu huyo ndie aliyemfundisha fisadi,hivyo Serikali yake walimu wote wataishi kifalme kwa kupata mishahara mikubwa na makazi bora.
*Askari polisi kupata mshahara mnono.
Ameendelea kuahidi kuwa askari polisi watapata mishahara minono kutokana na kazi kubwa ya kizalendo wanayoifanya usiku na mchana.
*Mabomba ya umeme kupita chini ya ardhi.
Aidha amesema kuwa Watanzania wamekua na asilimia ndogo ya kuishi kutokana na athari ya umeme kwasababu ya nyaya za umeme kupita juu ya nguzo,endapo upepo au kibunga kikitokea umeme unakatika,katika nchi za ulaya hali hiyo haipo,hivyo Serikali yake ya mchakamchaka itahakikisha nyaya zote za umeme zinapita chini ya ardhi kwa kutumia mabomba.
*Miundombinu ya barabara.
Nitaweka mashine za kuponda mawe na kusaga kokoto" Crusher"ili tujenge barabara za zege,tuachane na mambo ya lami ambayo ni mpango wa watu wachache ambao wanapiga fedha za miradi.
Katibu Mkuu AAFP Rashid Rai Awali Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Rai amesema kuwa utajiri wa Tanzania umetajwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kua kila Mtanzania atanufaika na utajiri huo kwa misingi ya kuondoa ujinga, umasikini na malazi.
Amesema kua kuna baadhi ya watangazaji wa vituo vya vyombo vya habari hapa nchini wamekua wakibeza sera za AAFP kua ahadi inazozitoa kwa Wananchi hazitekelezeki,nakusema kuwa wasipotoshe umma,kwani tanzania imejaliwa utajiri mkubwa ukiwepo wa Madini,maziwa,mito,mapoli,milima,wanyama na vingine vingi.
"Tuna utajiri mkubwa sana, utajiri huu umetajwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ukitafsiriwa kuwa uodoe maadui watatu ambao ni ujinga,umasikini na malazi,"amesema Rai.
Katika hatua nyingine mheshimiwa Mwiru amewaomba wananchi Oktoba. 29,Mwaka huu kumchagua Mgombea mwenza wa urais Chumu Abdallah Juma pamoja na mgombea ubunge jimbo la Kisarawe kupitia AAFP Husna Mzenga.

No comments
Post a Comment