MGOMBEA URAIS AAFP AHITIMISHA KAMPENI MOROGORO NA AHADI LUKUKI,WANANCHI WAMKUBALI WAAHIDI KUMPIGIA KURA ZA NDIO OKTOBA 29 MWAKA HUU
Na Mussa Augustine.Kilosa Morogoro
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Kunje Ngombale Mwiru amehitimisha kampeni zake katika kata ya Ludewa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro huku akitoa ahadi lukiki kwa Wananchi,ikiwemo kuweka helkopta moja kila Wilaya kwa ajili kutoa huduma za uokoaji inapotokea mafuriko.
Mheshimiwa Mwiru pia amesema kwamba atahakikisha kunakuwepo na huduma za uhakikia za Jeshi la zimamoto na uokoaji ili kuhakikisha nilakabiliana kwa haraka na majanga ya moto yanapotokea katika kata ya Ludewa na maeneo mengine Mkoani humo.
Miundombinu ya barabara.
Aidha ameendelea kusisitisza kuwa Serikali yake itahakikisha inajenga barabara kwa kiwango cha zege,pamoja na kuweka miundominu mizuri ya kilimo na ufugaji ili kuondoa migogoro inayotokana na wakulima na Wafugaji katika kata ya Ludewa na maeneo mengine Mkoani humo."Nitaweka mashine ya kuponda mawe" Crusher"tutaponda mawe na kusaga kokoto ili barabara zetu zote tuzijenge kwa kiwango cha zege,kwasababu tuna utajiri wa rasilimali za mawe katika Mkoa wetu wa Morogoro" amesema Mwiru.
Kuhusu Jeshi la Polisi na Jeshi la Akiba(Mgambo).
Amesema kuwa Jeshi la Akiba na Jeshi la Polisi Nchini linafanya kazi kubwa ya kulinda amani na mali za raia,hivyo akiwa rais atahakikisha askari wa majeshi hayo wanaishi kifalme kwa kuwezesha kupata maslahi yote ya msingi pamoja na mishahara. Maiti kudaiwa.
Amesema kuwa Serikali yake haitoruhusu daktari au mtu yeyote kuidai maiti hospitalini,nakwamba endapo itatokea kufanya hivyo basi daktari huyo atachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwekwa nayeye kwenye jeneza.
Maslahi ya Walimu.
Ameendelea kusema kuwa walimu wanafanya kazi kubwa lakini bado wamesahaurika katika kuboreshewa stahiki zao hivyo akingia madarakani atahakikisha anaboresha maslahi ya walimu.
Mafisadi kuliwa na mamba.
Aidha amesema kuwa siku akitangazwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuende Ikulu atahakikisha linajengwa bwawa la mamba Ikulu ili kuwatumbukiza mafisadi waliwe na mamba."Nitaongea na idara ya usalama wa Taifa inijengee bwawa la mamba ili mafisadi wote watafunwe na mamba,manake haiwezekani niende Ikulu halafu mafisadi niwaache nje wakifuga vitambi,nitawashghulikia ipasavyo."
Aidha Mgombea urais huyo amesema kuwa mabadiliko ya kweli yanahitajika,lakini pasipo na uzalendo hakuna mabadiliko,hivyo atahakikisha uzalendo unaendelea kufundishwa kwa jamii kwa kutumia Wazee wastaafu ambapo yataundwa madawati ya kufundisha uzalendo.Mikopo kwa akina mama wajasiliamali.
Amesema kuwa akina mama wamek
ua wakihangaishwa na Mikopo kausha damu,hivyo Serikali yake itatoa mikopo ya uhakiki ili waweze kukuza biashara zao.
Kila kijana kupewa power tiller.
Aidha ameongeza kuwa kila kijana mwenye umri wa kuanzia miaka 18,atapewa power tiller ili aweze kufanya shughuli za kuingiza kipato nakuachana na vitendo vya uhalifu vitokanavyo na kukata tamaa na hali ngumu za kiuchumi.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Rai amesema kuwa suluhu ya kuondoa migogoro ya Wakulima na Wafugaji ni kutumia sehemu ya maeneo ya akiba kuwapatia Wafugaji ili waweze kufuga bila kuingia kwenye mashamba ya wakulima.
"Tuna maeneo makubwa sana yaliyotengwa kama mapori ya akiba,hivyo tuyatumie maeneo hayo kuwapa wafugaji sehemu ya kufugia ili Wakulima waweze kulima na mazao yao yasiliwe na mifugo.Hata hivyo baadhi ya Wananchi.
wamezungumza kwa nyakati tofauti nakusema kuwa migogoro kati ya Wafugaji jamii ya Masai na Wakulima kata ya Ludewa Wilaya ya Kilosa unazidi kua mkubwa hadi kupelekea wakulima kupoteza maisha,wengine kupelekwa mahakamani lakini Serikali ya CCM iliyopo madarakani imeshindwa kutatua.
"Wamasai wanaua wakulima,wanabaka lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao, viongozi wa Serikali za mitaa na Vijiji wanakua upande wa Wafugaji hivyo sisi Wakulima hatuna mtetezi" amesema mmoja wa Wananchi hao aliejitambulisha kwa jina la Mariam Ndobele"mama majeshi"
No comments
Post a Comment