Zinazobamba

VYAMA VYA SIASA VYAHIMIZWA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU.


Na Mussa Augustine.

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,Jaji Francis Mutungi,amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu kuanzia August 28,Mwaka huu wakati wa kunadi wagombea.

Jaji Mutungi amesema hayo leo August 28,2025 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa ambapo amesisitiza kuwa vyama vya siasa vina wajibu wa kuendeleza misingi ya amani na mshikamano wa taifa,nakuachana na matumizi ya lugha za matusi au vitendo vyovyote vinavyosababisha uvunjifu wa amani.

“Hakikisheni mnafanya kampeni za kistaarabu wakati  wa kunadi wagombea wenu,jiepusheni kabisa na lugha za matusi,kashfa,uchochezi au vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu wa taifa letu,” amesisitiza Jaji Mutungi.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa amani na mshikamano ni urithi ulioachwa na waasisi wa taifa,hivyo viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi.

“Kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi. Uchaguzi si mwisho wa siasa wala maendeleo, turithishe amani hii kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo,”amesema.

Vilevile amewasihi viongozi hao wa vyama vya siasa kuacha kubabaika na upotoshaji unaoweza kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii na makundi mengine katika jamii,nakwamba uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa,hivyo wawe makini na taarifa zinazoleta taharuki.

“Mtaambiwa uchaguzi haupo,msikate tamaa, uchaguzi upo,na jambo kubwa zaidi ni kuhakikisha tunaingia kwenye uchaguzi huru na wa haki kwani ninyi ndio wakala wa kwanza wa kuhakikisha hilo linatekelezeka,” amesisitiza.

Kwa Upande Mwasilishaji kuhusu Sheria ya gharama za uchaguzi,wakili Edmund Mgasha amebainisha kuwa Kifungu cha kanuni za Uchaguzi 6(,1)(2) kinamtaka Msajili kuweka pingamizi dhidi ya Mgombea aliyeshindwa kuweka Wazi kiasi cha vyanzo vya gharama za Uchaguzi ndani ya siku 14 baada ya uteuzi


No comments