KITUMBUA AWANIA UBUNGE JIMBO LA CHAMAZI, AAHIDI NEEMA KWA WANANCHI
Na Mwandishi Wetu. Dar es salaam
Mgombea Ubunge Jimbo la Chamanzi kwa tiketi ya Chama cha Wakulima( AAFP )Shani Kitumbua amewaomba Wananchi ridhaa ya kuwa Mbunge wao kwani atatatua kero mbalimbali ikiwemo kuisemea barabara ya Kilungule ambayo ni Mbovu,uchache wa Shule na matukio ya kihalifu yanayotishia amani kwa raia
Hayo amebainisha leo August 19,2025 mara baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea Ubunge kutoka Ofisi ya Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bi Fortunata Shija,nakubainisha kuwa Jimbo la Chamanzi ni Jimbo jipya ambalo linahitaji kuboreshewa miundombinu muhimu ikiwemo kuwepo kwa za kutosha kwani kwa sasa Shule ni chache wanafunzi ni wengi.
"Mimi kama Mbunge nitakwenda kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri,na kuondokana na michango mbalimbali ambayo kwa sasa watoto Wetu wanalazimika kwenda nayo shuleni."kuondoa fedha wanazoagizwa Kila siku na waalimu siku za mapumziko wakisingizia ni masomo ya ziada"amesema Shani.
Vilevile amebainisha kuwa barabara ya Kilungule imekuwa sumbufu muda mrefu trafiki wameifanya ya kupigiwa hela kwa madereva daladala bajaji na Pikipikia
No comments
Post a Comment