WAKULIMA WASHAURIWA KUPIMA AFYA YA UDONGO WA SHAMBA KABLA YA KUANZA SHUGHULI ZA KILIMO
Na Mwandishi Wetu
Wakulima wameshauriwa kupima afya ya udongo wa shamba kabla ya kuanza shughuli za kilimo ili kupata uhakika wa virutubisho vilivyopo na vilivyopungua.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Agrami Afrika na Mzuri Afrika Shaaban Mgonja, katika maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl.Julius Kambarage Nyerere Dar es salaam.
Mgonja amesema kuwa kujua afya ya udongo kunapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija hivyo ni vyema wakulima wakafanya maandalizi mapema.Kwa upande wake afisa Kilimo wa kampuni hizo Salimu Msuya amesema kuwa wakulima watarajie huduma bora zaidi katika msimu ujao wa kilimo.
Wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, viongozi wa taasisi za serikali, wakulima na wafanyabiashara wa mnyororo wa thamani wa kilimo, wametembelea banda la kamluni hizo katika maonesho hayo.
No comments
Post a Comment