Sekta ya Usafiri Majini ina Mchango Mkubwa ukuaji wa Uchumi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) Nahodha Mussa Mandia amesema kwamba usafirishaji kwa njia ya Maji inachangua kwa kiasi kikubwa kwa ukuaji wa Uchumi hivyo ni lazima idhibitiwe na kulindwa kwa wivu mkubwa.
Taarifa hiyo ameitoa leo Julai 5,2025 wakati alipotembelea Banda la TASAC katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
"Njia ya Usafiri wa majini kinachoangaliwa ni usalama wa vyombo pamoja na mizigo inayoingia ndani pamoja na vyombo vidogo vya ndani vinavyotumia maziwa".amesema
"Nakuongeza kuwa katika usafiri wa bahari shehena kubwa zinazoingia ndio zinakwenda kuchochoe uchumi wa nchi katika kuongeza pato la Taifa."
"Bodi tumejipanga katika kushauri katika kuona matokeo yanaonekana katika kuendelea kulinda usalama wa vyombo vya majini pamoja na abiria katika vyombo vidogo kwenye maziwa"amesema Mandia.
Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuwekeza katika bandari mbalimbali na miradi hiyo itakuwa na matokeo mazuri katika katika kuendelea kuchochea maendelea kwa wananchi kwa uchumi wa mtu mmoja moja hadi taifa kwa ujumla .
Ameendelea kubainisha kuwa katika Maonesho ya yanayoendelea wananchi watembelee Banda la TASAC kupata elimu kuhusu sekta ya usafiri wa majini kwani ni muhimu kuwa na uwelewa mpana juu ya sekta hiyo.
No comments
Post a Comment