MLEMAVU WA MIKONO ANAECHORA RAMANI ZA NYUMBA KWA MGUU AISHAURI JAMII.
Na Mussa Augustine.
Mwanafunzi wa Mwaka wa pili wa chuo Cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA)Dodoma Joseph Joachim Mtei ambaye anatumia mguu kuchora ramani za Nyumba ameishauri jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu nabadala yake wawapeleke VETA wapate ujuzi utakao wasaidia kujikwamua kiuchumi.
Ushauri huo ameutoa leo Julai 4,2025 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Banda la VETA lililopo katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba,nakubainisha kuwa anasomea fani ya masuala ya uchoraji wa ramani na sasa anauwezo wa kuchora ramani ya aina yoyote.
"Naishukuru VETA kwa kunikubalia kujiunga kwa ajili ya kupata ujuzi huu,kwani hawakuona kwamba mimi nilemava ambaye sina mikono labda nitakua mzigo kwa walimu walinichukulia kama wanafunzi wengine"

Nakuongeza kuwa,Nilianza VETA Mwaka wa kwanza 2024 na sasa nipo Mwaka wa pili,nafurahia sana kwasabubu sasahivi nina uwezo wa kuchora ramani yoyote pasipo changamoto yoyote,sasahivi siwezi kuwa tegemezi tena kwa jamii au familia yangu,nauwezo wa kukitegemea mwenyewe."
Aidha amesema amekuja katika maonesho ya Kimataifa ya kibiashara maarufu kama Sabasaba kuwaonesha Watanzania wenzake kuwa wasiwafiche watoto wenye ulemavu,au wale wana viungo vyote lakini wamekata tamaa kwa kuona kwamba hawawezi kufanya chochote wanaweza kujiunga na VETA nakupata ujuzi wa fani mbalimbali.
"Wakija VETA hawawezi kukosa cha kufanya,watafanya kila kitu kwasabubu kama darasani wameona hakuna Cha kufanya,VETA wanafundisha kwa vitendo kwani hawa angalii uelewa wako wa darasani wana angalia matendo yako ambayo yatakufanya uweze kufanya kile ambacho wewe una uwezo nacho."amesema Joseph
Nakuongeza kuwa "Kwa mfano mimi hapa nimeenda VETA nikiwa sijui kabisa kuchora ramani za Majengo ila kwa vile walinipa Mafunzo na ujuzi sasa hivi nina uwezo wa kuchora ramani ambayo naweza nikaiuza kabisa nikapata kipato".
Hata hivyo Mtei amesema kwamba ramani haiwezi kuchorwa kwa siku moja na kuimaliza,inachukua muda,ili ramani ikamilike unaweza kutumia wiki moja,mbili hadi wiki tatu.



No comments
Post a Comment