Zinazobamba

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa DSM, Abuubakari Ally ( Boka) Achukua fomu ya Ubunge Kigamboni

Kada wa Chama Cha Mapinduzi - CCM, Abuubakari Ally ( Boka) amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni.

Abuubakari, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es salaam amefika katika ofisi za Chama wilaya kigamboni  akiwa na risiti ya malipo kwa ajili ya uchukuaji fomu aliyokabidhiwa na Katibu wa CCM wilaya stanley Mkandawile. 

Pamoja na kujihusisha na Siasa Boka ni mdau wa masuala ya afya na michezo nchini.

Wengine waliochukua fomu jimbo la Kigamboni ni Ally Mandai, Eng Hersi Said, na Dokta Henjewele.

No comments