Mbeto:Hotuba ya Rais Mwinyi akifunga Baraza la Wawakilishi zbar ni ya kimapinduzi
Chama Cha Mapinduzi kimesema hotuba ya Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kabla ya kulivunja alioitoa kabla ya kuvunja Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) ni ya kujivunia ufanisi wa sera na mkakati wa maendeleo ya kimapinduzi .
Chama hicho pia kimeitaja hotuba hiyo licha ya kugusa sekta muhimu na utendaji wa kazi za serikali, imeonyesha kupanda grafu ya maendeleo katika sekta za umma na sekta binafsi .
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanziabr , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis, amesema licha SMZ kufanya mageuzi ya kimapinduzi, Serikali kwa miaka mitano iliopita , imeleta tija kwa maendeleo yaliofikiwa.
Mbeto alisema utekelezaji wa kisera kwa miaka mitano toka mwaka 2020 -2025, SMZ imejiegemeza zaidi katika kukuza sekta za Utalii, Viwanda, Kilimo na Michezo na kasi ya ukuaji Uchumi wa Bluu ,pato la mtu na mapato ya Taifa .
Alisema kwa miaka mitano iliopita , SMZ chini ya Rais Dk Mwinyi, imefanikisha malengo ya kisera katika sekta za Elimu, Uwekezaji, Viwanda, Afya , Kilimo, Maji,Uvuvi na Biashara, Ajira ,Usafiri wa Anga na Tumefanikiwa kugawa vitalu kwa Makampuni ya Uchimbaji wa Gesi na Mafuta.
"Hotuba ya Rais Dk Mwinyi imewafumbua macho na masikio Wanasiasa wenye hulka ya ujuvi na ukaidi .Kila mtu amesikia mambo yaliofanikishwa na SMZ kwa miaka mitano iliopita "Alisema Mbeto
Aidha hotuba hiyo imetaja hatua zilizochukukiwa kimkakati lakini pia kuelezea matarajio na kufikia malengo mahususi kwa miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 .
" CCM imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na mkakati wa utendaji na utekelezaji wa kisera chini ya Awamu ya Nane. Chama kina imani kubwa na uongozi wa Rais Dk Mwinyi na watendaji wa Serikali yake " Alisisitiza Mbeto
Pia Katibu huyo Mwenezi ,alisema CCM kimefurahishwa kwa hatua madhubuti za SMZ za kuendeleza Umoja wa Kitaifa, kupinga ubaguzi wa aina yoyote na kutilia mkazo dhima ya kuwaunganisha wananachi.
Mbeto alisema ni aibu kubwa kwa Wanasiasa ambao mara kadhaa, wamekuwa wakipotosha ukweli wa mambo na kudaii hakuna kilichofanywa na SMZ kwa miaka mitano iliopita .
"Yote yalioahidiwa kisera na Rais Dk Mwinyi wakati wa kampeni za mwaka 2020 ametimiza ahadi zake .Ni kawaida ya CCM kuahidi na kutekeleza kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025" Alielez
Katibu Mwenezi huyo alisema kutokana na kupatikana na ufanisi wa kisera uliofanyika miaka mitano iliopita, CCM ina hakika ya kushinda tena uchaguzi Zanzibar ifikapo oktoba mwaka huu.
No comments
Post a Comment