WAZIRI MAVUNDE KUWA MGENI RASMI KONGAMANO LA WADAU WA SEKTA YA MADINI.
Na Mussa Augustine.
Taasisi ya huduma za usambazaji katika Sekta ya Madini Tanzania(TAMISA)imeandaa Kongamano litakalojadili changamoto na namna ya kuzifikia fursa zilizoko kwenye sekta ya madini.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei 14,2025 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano TAMISA Dkt.Sebastian Ndege amesema kuwa Kongamano hilo litafanyika siku ya ijumaa ya Mei 16,2025 huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Madini Anthony Mavunde.
Aidha amesema kuwa siku ya Kongamano hilo pia Kamati ya Mawasiliano itazinduliwa rasmi ili kuweza kuhabarisha umma na wadau wa sekta hiyo juu ya fursa zinazoweza kupatikana kupitia sekta ya Madini,kwani zitakua zikichapishwa kupitia tovuti(Website) ya TAMISA.
"Napenda kutoa Wito kwa wadau wote wa sekta ya Madini ikiwemo wafanyabiashara wa Madini na wachimbaji wa Madini kujiunga na TAMISA kwa lengo la kuwa na sauti moja katika kufikia malengo" amesema Dkt.Ndege
Peter KumalilwaKwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo,Peter Kumalilwa amesema kwamba uongozi wa Taasisi hiyo utahakikisha wazawa wana anzisha Viwanda vinavyohusiana na madini ili kuhakikisha Shilingi trillion 3.1 zinazotolewa na Makampuni makubwa ya madini hapa nchini,wazawa wachangie asilimia 20 au zaidi jambo ambalo litawafanya wajivunie kama Watanzania.
Pia Kumalilwa ametoa shukrani zake Kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuifungua sekta ya Madini katika soko la kimataifa na kuweka mikakati ya kuhakikisha wazawa wanapiga hatua kubwa katika sekta hiyo hapa nchini.
"TAMISA itakuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wazawa kufungua Viwanda vya madini, kuhabarisha wadau hususani wazawa kushiriki katika fursa zinazopatikana kupitia sekta hiyo,pamoja na kuwaunganisha wadau wazawa kuwa sauti moja na kufikia mafanikio yanayohitajika."Kumalilwa.
No comments
Post a Comment