Zinazobamba

WAKILI PETER MADELEKA AHAMIA ACT WAZALENDO.

Na Mussa Augustine 

Chama Cha Act Wazalendo kimemtangaza Peter Madeleka kuwa mwanachama mpya ambaye atasaidiana na jopo la Wanasheria wa Chama hicho katika kutetea haki za kisiasa kupitia utaalamu wake wa sheria. 

Akizungumza leo Mei 20,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa kumtambulisha na kumkabidhi katiba na kadi  ya chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka  Mchinjita amesema kwamba wakli Madeleka amekua msaada mkubwa wa kutetea haki za makundi yote katika jamii. 

Mchinjita ambaye pia ni Waziri Mkuu kivuli wa Act Wazalendo amesema kuwa wakili Madeleka anauwezo mkubwa wa kuimarisha nguvu katika vyama vya upinzani na kutoa matumaini ya kufikia malengo ambayo chama kimejiwekea. 
Kwa upande wake Wakili Madeleka ambaye amehama kutoka CHADEMA nakujiunga na Act Wazalendo amasema kuwa kudai Demokrasia ya kweli katika nchi, lazima kuwepo na njia mbalimbali ikiwemo kushiriki uchaguzi, kugombea, pia wakati mwingine kunakuwepo na vita kali ya kudai Demokrasia,hivyo amewataka  Act Wazalendo kushirikiana katika uchaguzi mkuu. 

Wakili Madeleka amesema vita kubwa ya vyama vya upinzani hapa nchini ni CCM pamoja na Serikali yake kwani imekuwa ikibinya Demokrasia kwa vyama vya upinzani nakuvidhoofisha ili visishike dola.

" Tunaenda kushiriki uchaguzi ili kupima na kujiridhisha  yale mabadiliko(Reforms)yanayosemwa yamefanywa na Serikali ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu kama ni kweli au la"amesema Wakili huyo msomi.

Nakuongeza kuwa" Mimi nimeamua kuja huku upinzani ili kuimarisha vyama vya upinzani ili dola ishindwe kuja huku kuvidhoofisha vyama hivi".


No comments