Zinazobamba

DKT.SAMIA MGENI RASMI TUZO ZA "SAMIA KALAMU AWARDS."



Na Mussa Augustine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za waandishi  wa habari za maendeleo zinazaofahamika kama SAMIA KALAMU AWARDS,zitakazotolewa April 29,2025 katika ukumbi wa Mabele,Mabeyo Complex Jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa  leo April 15,2015 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa  Chama Cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Dkt.Rose Reuben wakati akizungumza na waandishi habari ambapo TAMWA na TCRA wameandaa tuzo hizo.

Dkt.Reuben amesema kuwa tuzo hizo zimelenga kuhamasisha muandishi wa habari za maendeleo kujikita katika kufanya uchambuzi na utafiti wa kina,kuongeza maudhui ya ndani, kuzingatia weledi,maadili na uwajibikaji wa kitaaluma ili kukuza uzalendo na kujenga taswira chanya ya Taifa.

"Walengwa wa tuzo hizi ni waandishi wa habari,wachapishaji wa maudhui ya mitandaoni,ma afisa habari,watangazaji wa vyombo vya habari ambao walishiriki kwa kutuma kazi zilizorushwa ama kuchapishwa kupitia vyombo vyao"amesema Dkt Reuben

Nakuongeza kuwa "Tuzo hizo za "Samia Kalamu Awards" zinatokana na mafunzo yaliyotolewa mwaka jana 2024 kwa lengo la kukuza na kuendeleza uandishi wa habari za maendeleo nchini,washiriki wanaotarajiwa kupata tuzo hizo ni washiriki 79.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TAMWA ameendelea kubainisha kuwa tuzo hizo zimegawanyika katika makundi makuu matatu ambapo kundi la kwanza linahusisha tuzo maalumu za kimataifa ambazo ni pamoja na tuzo ya chombo Cha habari mahiri kitaifa,tuzo ya wanahabari wabobevu,tuzo ya Afisa habari mahiri wa serikali,Tuzo ya mwandishi wa habari mahiri kitaifa  na tuzo ya uandishi wa habari za matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha amesema kundi la pili linajumuisha tuzo kwa vyombo vya habari vya Televisheni, vyombo vya habari mtandaoni, Redio ya kitaifa, Magazeti na Redio za kijamii.

Huku kundi la tatu ni tuzo za kisekta zitakazotolewa kwa waandishi wa habari waliobobea katika kuandika makala za maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, maji, nishati, mazingira, jinsia, wanawake na makundi maalumu, ujenzi, viwanda na biashara, maliasili na utalii,

mifugo na uvuvi, uchumi wa buluu, kilimo, utamaduni, sanaa na michezo, TEHAMA na ubunifu, mazingira, ardhi na makazi, madini, fedha na uchumi, vijana, elimu na uwekezaji.

"Tukio la tuzo hizo litarushwa mubashara kupitia vituo mbalimbali vya Televisheni,Redio, na mitandao ya kijamii ili kuwawezesha wananchi wote waliowapigia kura waandishi na vyombo vya habari kufuatilia matokeo na utoaji tuzo" amesema Dkt Reuben 

" Nakuongeza kuwa washindi watatunukiwa zawadi mbele ya mgeni rasmi kama ishara ya kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika ustawi wa taifa.


No comments