Zinazobamba

HANSPAUL GROUP YAIUNGA MKONO SERIKALI MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

Na Mussa Augustine.

Kampuni ya Hanspaul Group ambayo inatengeneza magari ya kitalii yanayotumia teknolojia ya  Nishati ya Umeme,imejipanga kuendelea kuiunga mkono Serikali katika jitihada za matumizi ya nishati safi.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 11,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji Kampuni hiyo Satbir Singh Hanspaul wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonesho ya nane ya kimataifa ya Utalii( S!TE) yanayofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam

Aidha amesema kuwa kwa sasa Serikali imeweka Mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hivyo kampuni ya Hanspaul Group imefanikiwa kutengeneza teknolojia ya matumizi ya nishati ya Umeme kwenye magari ya Utalii,ili kuweza kuwa na Utalii wa kijani( Green Tourism).

"Sisi tupo tayari kuiunga mkono Serikali yetu ,Namshukuru sana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Utalii maana wametengeneza Mfumo Mzuri sana kwa Tanzania," amesema

Nakuongeza kuwa " Tanzania imekuwa na amani kubwa ,Utalii bila amani hauendi lazima ziende pamoja ,hivyo sisi kama Hanspaul Group tupo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Aidha amesema kuwa Kampuni hiyo inapatikana Mkoani Arusha ,nakutumia fursa hiyo kuwakaribisha watu wote wanaotamani kutumia magari hayo yenye teknolojia ya kisasa ya matumizi ya nishati ya Umeme Nchini.

" Tumefanikiwa Kuuza magari haya katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Namibi mpaka Ethiopia ,tunaendelea pia kutafuta masoko katika nchi zingine" amesisitiza Satbir 

Akizungumzia ubora wa magari hayo, Satbir Hanspaul amesema kuwa magari hayo yameifanya Tanzania kuwa katika nchi ambazo zinajari mazingira,nakwamba bidhaa hiyo inaifanya Tanzania kuwa katika soko la juu.

"Utalii ni moja ya kipaumbele  kwa Nchi yetu,ina leta fedha za kigeni hivyo sisi kama Hanspaul Group tumeamua kutumia bidhaa hii ya green tourism ili kuisaidia serikali kutekeleza adhma yake ya kutumia Nishati safi na salama ili kuhifadhi Mazingira.




Hakuna maoni