Zinazobamba

NLD YAZINDUA OPARESHENI "FYEKA CCM 2024/2025",YAPOKEA WANACHAMA WAPYA


 Na Mwandishi Wetu.

Chama Cha National League For Democracy (NLD) ni kama  vile kimeanza makeke baada ya kumtambulisha Mwanachama nguli kutoka ACT Wazalendo,Mariam Sijaona na kuzindua Operesheni  inayoitwa Fyeka Chama Cha Mapinduzi( CCM) 2024/2025, watakayoitambulisha katika mikoa 10.

Sijaona, kabla ya leo kutambulishwa na kukabidhiwa kadi, alikuwa ni Naibu Katibu Mwenezi Ngome ya Wanawake na Mjumbe Halmashauri Kuu Kanda ya Pwani ACT Wazalendo.

Katika utambulisho huo wa baadhi ya wanachama wapya ambao wamejiunga na NLD uliofanyika Septemba 29,2024 jijini Dar es Salaam, pia alitambulishwa Scola Kahana aliyekuwa Mgombea Ubunge Kibaha Mjini 2020 kutokea chama Cha Allience for Democratic Change (ADC).

Doyo katika utambulisho huo wa wanachama wapya na uzinduzi wa Operesheni ya mpya watakayokwenda kuitambulisha katika mikoa 10, alisema watakwenda kufanya siasa  safi na si za kutukana watu.

"Uwezi kufanya vizuri katika majukwaa ya siasa na kuchukua nafasi za uongozi katika chaguzi kwa kutukana watu, tunaipenda nchi yetu na tunawasihi wanasiasa wengine kufanya siasa safi ili kulinda amani ya nchi yetu.

" Siasa lazima zifanyike katika mazingira yanayoheshimika, wanasiasa tuheshimiane tusifanye kiburi kwa viongozi ambao wako madarakani, kwa uelewa wangu siasa ni tunu inayosogeza  maendeleo kwa wananchi "alisema.

"Juzi tunasikia kuna kongamano lilifanyika nchini la wanawake wa chama kimoja cha siasa, wakasema maneno mabaya kwa  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  yenye tafsiri mbaya  kwenda kumtuhumu kiongozi wa nchi huko ni kuikosea siasa za Tanzania na wananchi awawezi kuendeshwa kwa siasa za namna hiyo hivyo ni muhimu kuwa wastaarabu"alisema.

"Chama Cha NLD kinakuja kuonesha njia ni chama mbadala kinachokwenda kushika dola kwani tunasera na itikadi nzuri, tunaamini katika haki na uzalendo "alisema.

Aidha  ameendea kuiomba Ofisi ya Rais Tawaka za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuongeza muda wa kufanya kampeni kwani muda wa wiki moja ambao umepangwa hautoshi kutokana hatua za kufanikisha huo kubanana.

"Tunaiomba TAMISEMI irekebishe ratiba ya Uchaguzi wa Serikali siku za mchakato ziongezwe ili vyama vya siasa viweze kujipanga vizuri"alisema

Akizungumzia kuhusu Programu waliyoizindua Doyo amesema wamejipanga kutembea mikoa 10 ikiwemo Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma,Mbeya, Singida, Dodoma,Mwanza na Kagera.

Alisema kupitia programu hiyo watategeneza  wagombea ambao wataweza kushindana katika nafasi mbalimbali za uchaguzi kuanzia Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kwa hoja.

Naye, mwanachama mpya aliyetambulishwa leo, amesema " Leo nimejiunga rasmi NLD bila kushawishiwa na mtu na sijafukuzwa ACT na hakika watashaangaa. 

"Nilifanya kazi kubwa kukijenga ACT hususan katika mikoa ya kusini na kwingineko CCM wananijua vizuri na wananigwaya, naamini Kwa ushiriakiano uliopo tutafanya vizuri katika ujenzi wa chama na katika chaguzi za Serikali za Mitaa," amesema Mariam 


Hakuna maoni