Zinazobamba

MNG'AGI ALIA NA SERIKALI KUHUSU MUDA WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Na Mussa Augustine.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi( CUF) Wilaya ya Temeke Said Mng'agi ameiomba serikali kuongeza muda wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa madai kuwa muda wa siku saba uliopangwa hautoshi.

Akizungumza na Fullhabari Septemba 26, 2024 amesema kuwa muda wa siku saba unasababisha wananchi kukosa fursa ya kusikiliza wagombea wanapojinadi sera zao katika kuchukua mamlaka ya uongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji.

Aidha ameishauri serikali kupitia TAMISEMI kuongeza muda angalau siku kumi na nne(14) kama ilivyokua hapo awali kwani itasaidia kupata muda wa kutosha wagombea kunadi sera zao .

"Mimi wakati nikiwania uongozi Serikali za Mi, tulikua tuna zunguka wiki mbili kufanya Kampeni na kujitangaza,muda huo angalau ulikua unatosha" amesema.

 
Aidha amesema kuwa haoni mantiki ya Serikali kuweka siku saba nahuku programu ya uchaguzi huo  hufanyika kwa muda wa siku kumi na nne.

Akizungumzia maandalizi ya Uchaguzi huo katika Wilaya ya Temeke, Mng'agi amesema kuwa CUF imejipanga vizuri kuhakikisha inasimamisha wagombea katika kila Mtaa ili kuweza kupata Wenyeviti wa Mitaa wengi kupitia chama hicho.

"Mimi kama Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke,nimefanya ziara kwenye kila kata kuhamasisha kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha wakati litakapofika daftari la kudumu la wapiga kura  la Mtaa ili waweze kuchagua kiongozi wanaomtaka kulingana na sera za chama anazozitangaza," amesema.

Aidha amesema kuwa chama cha CUF bado hakijapoa kama wanavyodhani baadhi ya watu,nakwamba bado kinafanya shughuli zake  kama kawaida.

"Ndugu mwandishi  ukiangalia chama ambacho kimekua kikifanya uchaguzi kuanzia ngazi za Mitaa ,kata mpaka Wilaya ni chama cha Wananchi CUF,katika upinzani sijaona chama kingine" amesisitiza

Vitendo vya Mauaji na Utekaji
Mwenyekiti huyo amelaani vikali matukio ya utekaji na Mauaji yanayoendelea Nchini humo,nakusema kuwa Serikali ina mkono mrefu wa kuhakikisha inakomesha matukio hayo.

"Ni aibu kwa Taifa letu kua na mauaji kama haya ,dunia haitutazami vizuri,napenda kuishauri Serikali kuchukua hatua stahiki kuhakikisha vitendo vya  mauaji na utekaji vinakomeshwa.

Nakuongeza kuwa" Vitendo hivyo vina ashiria kutoweka kwa amani kwasababu tumezoea huko nyuma hapakua na vitu kama hivi,mamlaka za usalama ikiwemo Jeshi la Polisi vichukue hatua kukomesha vitendo hivi.

Hata hivyo amesema kuwa licha ya Viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani kwenye maeneo mbalimbali ,vitendo vya utekaji na mauaji vinaendelea kutokana na kukosekana kwa hali ya ushirikishwaji na Demokrasia ili kuhakikisha Watanzania wanakua na umoja,nakwamba Serikali ijipange kukomesha hali hiyo.








Hakuna maoni