Zinazobamba

SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU MZUMBE TAWI LA TEGETA WAJENGEWA UWEZO NAMNA YA KUWA VIONGOZI BORA

Uongozi wa Serikali ya wanafunzi chuo Kikuu cha Mzumbe (MUSO) Tegeta umetakiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa na wanafunzi wenzao na siyo kuwa sehemu ya kutengeneza Migogoro, kwa kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya wanafunzi na uongozi wa Chuo.

Hayo yamesemwa mapema leo Juni 22, 2024 na Kaimu Mkuu Ndaki ya Dar es salaam Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Joshua Mwakujonga wakati akifungua mafunzo Maalum ya siku moja kwa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi MUSO chuoni hapo.

Aidha Dkt. Joshua amewataka viongozi hao kuweza kuwa wa kwanza kufuata sheria pamoja na taratibu za chuo, ili wanafunzi wengine waweze kujifunza kutoka kwao kwani serikali ya wanafunzi ndio msingi wa kujifunza uongozi na hatimaye baadae kuja kuwa viongozi bora katika nyanja mbalimbali.

"Serikali ya wanafunzi ndio tanuru la kuwapika viongozi na hata ukiangalia wanasiasa na viongozi wengi wa vyama na serikali  chimbuko lao walianzia kuwa viongozi mashule na vyuo mbalimbali" alisema Dkt. Joshua

Ameongeza kwa kusema kuwa wao kama Chuo Kikuu Mzumbe wamejipanga kukabiliana na suala la "uthibiti" kwani hivi sasa kumekuwa na ushindani mkubwa wa vyuo na ndio maana wanajitahidi kutoa elimu bora, ili pia hata wanafunzi wao wanaowazalisha waweze kuuzika katika soko la ajira mbalimbali.

Ameendelea kwa kusema kuwa mafunzo hayo ni endelevu na huwa yanafanyika zaidi ya mara moja kwa mwaka baada ya uchaguzi na kupatikana viongozi wapya, lengo likiwa ni kuwaongezea uwezo ili waweze kuwa na uongozi imara wenye mashirikiano mazuri kati yao na waadhiri wao.

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo ambae pia ni mshauri wa wanafunzi Dada Zita Mnyanyi amesema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwatengenezea msingi mzuri wa uongozi wakiwa bado vijana, na pia ni utaratibu wao kama chuo kuandaa mafunzo kama hayo kila unapoingia uongozi mpya ili waweze kuongoza katika misingi inayotakiwa.

Ameongeza kwa kusema kuwa wameona kuna tija ya kuwapa mafunzo kwa kuwa wao ni daraja linalounganisha kati ya uongozi mkuu wa Chuo (Waadhiri) pamoja na wanafunzi kwani wao ni sauti ya wengi waliopo nyuma yao na endapo kutakuwa na shida wajue wataanzia wapi kutafuta suluu mpaka kufika ngazi za juu.

Aidha ameendelea kwa kusema kuwa waendesha semina hiyo ni waadhiri wa chuo hicho kwa kushirikina na ofisi ya Mshauri wa wanafunzi, na baadhi ya mambo yaliyokuwa yakifundishwa ni masuala ya Uongozi, fedha na bajeti, Mawasiliano na maadili, Migogogro na namna ya kuipatia ufumbuzi pamoja na usimamizi kwa watendaji wa chini yao.

Na mwisho amemalizia kwa kusema kuwa mafunzo hayo yameendelea kuwa ni nyenzo muhimu sana kwa wanafunzi, kwani wameona kwa baadhi ambao wamepita baada ya mafunzo huwa kunakuwa na mrejesho mzuri na hii inaonyesha kwa kiasi gani mafunzo hayo yameweza kuleta tija kwao.

Naye Rais wa serikali ya Wanafunzi chuoni hapo Kosta Mash amesema kuwa anashukuru sana kwa waadaaji wa mafunzo na pia anatoa ahadi kuwa yeye na serikali yake watatekeleza yale yote waliyofundishwa ili kuweza kutengeneza serikali iliyo bora.

Ameongeza kuwa yeye na serikali yake ya mwaka 2024/25 itakuwa ni ya mfano kwa kufuata sheria na taratibu zote za chuo kama walivyofundishwa, na kusema kuwa hawataweza kuwaangusha wale wote waliowaamini kwa kuwachagua na kwamba wasiwe na wasiwasi wamechagua watu sahihi wa kuwaongoza.

Kaimu Mkuu Ndaki ya Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Joshua Mwakujonga akiongea na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuoni hapo(MUSO) wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo kuwa Viongozi bora.

Mratibu wa mafunzo ambae pia ni mshauri wa Wanafunzi Dada Zita Mnyanyi kitoa wasilisho lake kwa Serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu Mzumbe mwaka 2024/25.

Rais wa serikali ya Wanafunzi chuo Kikuu Mzumbe Tegeta Kosta Mash akipokea cheti kutoka kwa Mratibu wa Kituo cha Tegeta Dkt. Janeth Swai baada ya mafunzo ya kujengewa uwezo



Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Kanti Mtey akiongea na Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe katika semina ya kuijengea uwezo serikali mpya ya wanafunzi iliyoingia mwaka huu 2024.

Mafunzo yakiendelea kwa Viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu Mzumbe Tegeta.
Mhadhiri wa Chuo kikuu Mzumbe Tegeta Henry Lung'aro
 aliwasilisha mada ya Mawasiliano pamoja na maadili kwa Viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuoni hapo.
Mratibu wa Kituo cha Tegeta Dkt. Janeth Swai, akifunga Mafunzo  ya siku moja wa kuwajengea uwezo Viongozi wa Serikali ya Manafunzi Chuo kikuu Mzumbe (MUSO) kituo cha Tegeta.

No comments