• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Advertise

Full Habari
ads header
    • KITAIFA
    • KMATAIFA
    • BIASHARA
    • SIASA
    • MICHEZO
  • Zinazobamba

    Home / Unlabelled / RAIS WA JAMHURI YA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA.

    RAIS WA JAMHURI YA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA.

    mashala 08:13:00


     

        Balozi Dkt. Samweli Shelukindo 

     

    Na Mussa Augustine.

     Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na Mwenyekiti wa Taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA), Mh. Umaro Sissoco Embaló anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu hapa nchini kuanzia Juni 21 hadi 23 Mwaka huu.

     Hayo yamesemwa leo Juni 20,204 Jijini Dar es Salaam na  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samweli Shelukindo wakati akizungumza na waandishi wa habari,nakubainisha kuwa  ziara hiyo inalenga  kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Guinea Bissau pamoja na kuibua maeneo ya kushirikiana katika sekta mbalimbali za kimkakati za nchi hizo mbili.

     Balozi Dkt Shelukindo amesema ushirikiano huo unahusisha uzalishaji wa zao la korosho, ushirikiano katika masuala yanayohusu udhibiti wa ugonjwa wa Malaria kupitia Taasisi ya ALMA, na ushirikiano katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

     “Kupitia ziara hiyo Tanzania na Guinea Bissau zimedhamiria kuimarisha na kuinua kiwango cha ufanyaji biashara na uwekezaji hususan kupitia Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) ambapo nchi zote mbili zimeridhia uanzishwaji wa eneo hilo”amesema

     Nakuongeza kuwa “Tunatarajia kuwa ziara hii ,itatoa fursa kwa nchi hizi mbili kujadili kwa kina namna ya kuendelea kupambana na kudhibiti ugonjwa hatari wa Malaria kwa kuzingatia kuwa, Mhe. Rais Umaro Sissoco Embaló ni Mwenyekiti wa ALMA ,taasisi ambayo ilianzishwa mwaka 2009 na Viongozi wa Nchi zote 55 za Afrika kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030

     Aidha amesema kuwa  wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwaka 2023, Mwenyekiti wa ALMA, Mhe. Rais Umaro Sissoco Embaló alizitambua nchi 7 ikiwemo Tanzania kwa kubuni matumizi bora ya Kadi ya alama ya ALMA (ALMA Scorecard) inayosisitiza uwajibikaji na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambapo kupitia mpango huo, Tanzania ilitoa mafunzo kwa Wabunge, Viongozi mbalimbali na watoa huduma za Afya kuhusu namna ya kutumia kadi hiyo ya alama katika kuhamasisha uwajibikaji na utoaji elimu kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

     Hali kadhalika amesema kuwa  Guinea Bissau imejikita katika uzalishaji wa zaola Korosho ambalo nchi hiyo huuza zaidi nchini India huku thamani ya uuzaji nje wa zao hilo inafikia takribani asilimia 90 ambapo pia zao hilo ni chanzo kikuu cha mapato kwa wakulima wadogo wa nchi hiyo na asilimia 80 huchangia asilimia 10 ya Pato la Taifa la Guinea Bissau.

     Balozi Dkt Shelukindo amesema kupitia ziara hiyo, suala la uzalishaji wa zao la Korosho ambalo pia hulimwa hapa nchini hususan katika mikoa ya Kusini ikiwemo Mtwara na Lindi litajadiliwa kwa kina ili kuhakikisha linapewa kipaumbdele katika ushirikiano wa kibishara na nchi hizo.

     Mh.Rais Umaro Sissoco Embaló na ujumbe wake watawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mh. January Makamba Juni 21 Juni 2024.

     Mheshimiwa Rais Embaló atapokelewa rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 22 Juni 2024 na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Baada ya mapokezi hayo, viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye watashiriki katika mazungumzo rasmi kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Guinea Bissau, na baadaye kuzungumza na Waandishi wa Habari kuelezea masuala muhimu yaliyojiri katika mazungumzo yao.

     Sanjari  na hayo Mh. Rais Embaló na ujumbe wake atatembelea Miundombinu ya Reli ya Kisasa katika Kituo cha Stesheni jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) na taasisi ya Muungano wa Viongozi wa Afrika katika Kudhibiti Malaria (ALMA).

     Ziara hiyo ni mwendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali ili kuinufaisha nchi kiuchumi ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo.

     


    RAIS WA JAMHURI YA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA. RAIS WA JAMHURI YA GUINEA BISSAU KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI TANZANIA. Reviewed by mashala on 08:13:00 Rating: 5
    Share This
    Facebook Twitter Google+

    No comments

    Post a Comment

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    Ads

    Popular Posts

    • MATOKEO YA MTIHANI HAYA HAPA NI YALE YALIOTANGAZWA NA NECTA LEO,BOFYA HAPA KUJUA
    • MIZENGO PINDA AMUHURUMIA MBUNGE KAWAWA,HALI YAKE YASHTUA WENGI TIZAMA PICHA HIZI
      MIZENGO PINDA AMUHURUMIA MBUNGE KAWAWA,HALI YAKE YASHTUA WENGI TIZAMA PICHA HIZI
    • WAISLAM WAONYWA,WAAMBIWA MANENO KUNTU,SOMA HAPA KUJUA
      WAISLAM WAONYWA,WAAMBIWA MANENO KUNTU,SOMA HAPA KUJUA
    • SERIKALI YAZINDUA MAFUNZO YA MTANDAO YA AFYA MOJA (ECHO)
      SERIKALI YAZINDUA MAFUNZO YA MTANDAO YA AFYA MOJA (ECHO)

    Total Pageviews

    Recent Posts

    Tangazo

    Labels

    • Afya
    • Biashara
    • Burudani
    • Dini
    • Elimu
    • Jamii
    • Kijamii
    • Kimataifa
    • Kitaifa
    • Mahakama
    • Michezo
    • Siasa

    Facebook

    Followed Blogs

    • Michuzi
    • Dar24
    • MPEKUZIHURU

    KWA MATANGAZO

    WASILIANA NA UONGOZI WA FULLHABARI KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO:

    0714 099 486
    0689 311 158

    Theme By Sora Templates | Designed By Mbinda Technologies (T) Ltd | Copyright © Beta Media Consultance Lmited