Usiyoyajua kuhusu nia ya Siro kukagua mafunzo yanayotolewa madras, Sunday schools
Na Mwandishi wetu
Ni kweli kuwa Jeshi la Polisi
Tanzania limesema litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo
wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools)
kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.
Umewashawahi kujiuliza kwa nini
ni muhimu sasa, Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania, IGP Simon Sirro amefichua kuwa wamejifunza mengi nchini Rwanda na
kuamua kuyatekeleza nchini Tanzania.
Ameeleza hayo wakati akizungumzia
ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko,
hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.
“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano
haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo
yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni
mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba
watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi
kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za
elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au
yanawabomoa vijana.
Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo
itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio
lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na
shughuli zake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni