Tanzania yapokea msaada wa Sh 67.82 kutoka Ujerumani kusaidia Mradi wa Uhifadhi wa Maliasili na Mifumo ya Ikolojia
Mkataba wa msaada
huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya
Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani wa Umoja wa Afrika
Christoph Tskens, kwa niaa ya Serikali ya Ujerumani.
Akizungumza katika
hafala utiaji saini mkataba huo Katibu Mkuu huyo amesema kuwa fedhaizo
ziatatumika kwa ajili ya kuendeleza na kuhifadhi maliasili katika Hifadhi ya
Serengeti pamoja na kugharamia mradi wa uhifadh endelevu wa maliasili na mifumo
ya Ikolojia katika maeneo ya Ushoroba wa Katavi-Mahale.
" Lengo la
mrdai wa Serengeti ni kuchnagia maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na usimamizi
endelevu wa maliasili katika Wilaya ya Bariadi, Bunda, Serengeti, na Ngorongoro
wakati wa mradi wa Ushoroba wa Katavi-Mahale unalenga usimamizi wa maliasili
sambamba na kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhusisha matumizi bora ya ardhi
na utoaji wa hatimiliki za kimila," amesema Tububa.
Amebainisha kuwa
kiasi cha Sh Bilioni 21.7 zitatumika katika mradi wa kuendeleza a kuhifadhi
maliasili katika hifadhi ya Serengeti na Sh Bilioni 46.12, zitaenda kwenye
mradi wa uhifadhi endelevu wa maliasili na mifumo ya Ikolojia ushoroba wa
Katavi- Mahale.
Kwa upande wake,
Blozi wa Ujerumani nchini tTanzania, Regine Hess ameahidi kuwa nchi yake
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboreshamazingira ili kukabiliana
na mabadiliko ya Tabia ya nchi ambayo hayaiathiri Tanzania pekee bali duni akwa
ujumla.
Nae Mkurugenzi wa
Benki ya Maendeleo ya Ujerumani wa Umoja wa Afrika, Tiskens amesema kuwa benki
hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya utalii kwa kuboresha
maeneo ya uhifadhi pamoja na kuziweezsha jamii zinazozunguka maeneo hayo li
waweze kuzitunza hifadhi hizo.
Tanzania imekuwa
ikinufaika na ufadhili wa Serikali ya Ujerumani katika sekta za afya, maji,
nishati, matumizi endelevu ya maliasili na usimamizi bora wa fedha za umma
amabpo kiasi cha Sh Bilioni 678.54 zilitolewa kwa ajili ya miradi inayoendelea
kutekelezwa na shilingi Bilioni 599.23 kwa miradi iliyokamilika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni