Serikali kuendelea kutoa mafunzo ufundi stadi kwa vijana kupambana na ukosefu wa ajira
Baadhi ya vijana walioshiriki Kikao cha Kujadili na Kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) |
Serikali imesema
itaendelea kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana nchi nzima ili kukabiliana na
tatizo la ajira huku ikibainisha takwimu zinaonyesha mahitaji ya vijana
inaongezeka siku hadi siku na kwamba asilimia 31.5% ya watu waliopo nchini ni
vijana sawa na asilimia 57% ya nguvu ngazi ya taifa.
Hayo yamesemwa
jijini Dar es Salaam na Ofisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Julius Tweneshe
katika Kikao cha kujadili Rasimu ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana
kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee kikiwakutanisha vijana kutoka mikoa ya Dar es
Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Tanga.
Amesema kuwa
Serikali ina dhamira kukabiliana na changamoto ya ajira hivyo mafunzo
yanayoendelea kutolewa kwa vijana yatawasaidia kuweza kujiajiri katika
sekta mbalimbali
"Serikali
katika kuhakikisha kundi hili linapewa kipaumbele kuweza kuchangia Uchumi wa
nchi Serikali imeunda sera vijana ya Mwaka 1996 inayo wahiza vijana
kujitolea" amaesema Tweneshe.
Amebainisha kuwa
katika Marekebisho ya sera hiyo iliyofanyika 2007 sera hiyo ililenga
kutenga maeneo maalumu ya kiuchumi kwa vijana.
Amesisitiza kuwa
kiwa katika kuhakikisha masuala ya vijana yanazingatiwa Serikali imetenga
asilimia 10% kwa ajili ya mikopo kwa vijana kwa kila halmashauri ili
kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa
katika sera mwaka huu imelenga kutatua changamoto za kukuza ujuzi kwa ngazi
kitaifa na kimataifa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa community Harb Foundation, Paul Makoe amesema rasmu ya awali ni
tofauti na waka huu ambayo imeongezewa vipengele vya watu wenye ulemavu na
ajira zimeanza kuwainua vijana.
Nae Kijana Tatu
Sultan mwenye ulemavu wa ngozi amependekeza kuwa vijana wenye makundi maalum
wapewe kipaumbele katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya ajira ili
kuondokana na vitendo vinavyashiria unyanyapaa kwa jamii inayowazunguka.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni