Mnadhimu Mkuu JWTZ amwagia sifa Kapteni Selemani Semunyu, wapongezwa kulitangaza jeshi kupiyia michezo
Afisa Habari wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Kapteni
Selemani Semunyu na askari walioibuka na Ushindi katika Mashindano ya
Kombe la Mkuu wa Majeshi wapongezwa kwa Mafanikio na Kulitangaza Vyema Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika Michezo.
Hayo yalisemwa Jana na Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Mathew Mkingule wakati
wa hafla ya ufungaji Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa Mchezo wa Golf.
” Nimpongezea Kapteni Semunyu Kama hamjui umahiri
wake ulianza kuonekana akiendesha kipindi Cha Dk 45 ITV na Sasa tunajivunia
kuwa na mtu wa aina yake.” Alisema Luteni Jenerali Mkingule.
Alisema tunatambua uwezo wake ndio maana Jeshi
likaona umujimu kuwa nae na Umahiri huo tumekuwa tunauona katika majukumu yake
katika kuitangaza JWTZ na nchi kwa Ujumla kupitia Vyombo vya Habari.
Aliongeza kuwa kutokana na Umahiri wake na
jitihada za kulitangaza jeshi na nchi hasa katika Michezo atafikisha kwa Mkuu
wa Majeshi taarifa ya kazi Nzuri inayofanywa sambamba na Wachezaji wa
Gofu Askari walioshinda Mashindano haya.
Aidha aliwapongeza Askari wa Klabu ya Golf ya
Lugalo walioshinda katika mashindano hayo kwani alisema imedhihirisha
namna walivyojituma na hatimaye kushinda.
“Askari mlioshinda mmefanya kazi kubwa ya kuletea
sifa JWTZ na Taifa kwa Ujumla hakuna budi kupongezwa sambamba na Mwenyekiti kwa
kuwalea vizuri kimchezo mpaka kufikia hapo” Alisema Luteni Jenerali Mkingule.
Pia alisema JWTZ ipo katika mpango wa kuhakikisha
inajenga Viwanja vya Golf katika Mikoa Mwingine Kama vile Arusha na Iringa eneo
la Mafinga.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Klabu
ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo aliomba Jeshi
kukamilisha ahadi ya Ujenzi wa Uwanja Jijini Dodoma.
Aidha alisema Kama Klabu imejiandaa kutengeneza
wataalam watakaofundiaha mchezo huo mahala popote itakapo hitajika.
Mshindi wa Jumla wa Mashindano hayo Ni Mchezaji
Victor Joseph kutoka Klabu ya Dar ES Salaam Gymkhana.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni