“Ampasua mtoto wa kaka yake miguu na kumtenganisha vipande viwili na kutoa maini ili ayapike”
Na Joseph Lyimo
UKATILI wa kijinsia unakinzana na haki za binadamu, utu wa mtu unapashwa
kudhamini kwani kila mtu ni sawa chini ya sheria haijalishi ni mwanaume,
mwanamke au mtoto.
Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Manyara, yamekuwa yakitokea mara
kwa mara kwa vyombo vya habari kuripoti ikiwemo vipigo kwa wanawake na watoto
hadi kusababisha majeruha au vifo.
Jeshi la polisi mkoani Manyara, kupitia dawati la jinsia wamekuwa wakitoa
elimu kwa jamii kutochukua sheria mkononi na kushirikisha vyombo vya sheria
lakini suala hilo llimekuwa bado halijawaingia watu ipasavyo kwani matukio ya
ukatili kwa wanawake na watoto bado yanaripotiwa kutokea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Merrison
Mwakyoma amesema matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakitokea mara kwa
mara japokuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii ili kukomesha hayo.
Kamanda Mwakyoma amesema hivi karibuni kulitokea matukio zaidi ya 10 ya
ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo wanawake na watoto walifanyiwa na
watuhumiwa wanashikiliwa polisi au kufikisha mahakamani.
Ametaja baadhi ya matukio hayo ni Agosti 19 mwaka huu kwenye mtaa wa
Silaloda mjini Mbulu, Harold Hhando (35) alimuua mtoto wa kike wa kaka yake
Emmanuela Hhando (13) na kumpasua katikati ya miguu na kumtenganisha
vipande viwili na kutoa maini ili ayapike.
Amesema Agosti 23 mwaka huu mkazi wa kijiji cha Kiongozi wilayani Babati
Lucas Mangu (46) alimuua kwa kipigo mke wake Anna Kisino (41) kwa wivu wa
kimapenzi hata hivyo naye Mangu alijinyonga.
“Tukio lingine la ukatili kwa mtoto lilitokea Septemba 12 mwaka huu mjini
Babati ambapo Janeth Vicent alimchoma moto sehemu mbalimbali za mwili motto
wake wa miaka mitatu baada ya kumuomba fedha mpita njia,” amesema kamanda
Mwakyoma.
Amesema Septemba 4 mwaka huu kinyozi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani
Simanjiro, Athuman Rajabu (57) alimlawiti mvulana mwenye umri wa mika 16 ambaye
ni mlemavu wa kusikia na kuzungumza.
Mkazi wa Dagailoi mjini Babati, John Paulo amesema matukio ya wanaume
kupiga au kuwaua wanawake kutokana na wivu wa kimapenzi yamekuwa yakijirudia
mara kwa mara.
Paulo amesema ni bora kumuacha mwanamke kuliko kumpiga au kumsababishia
kifo kwa wivu wa mapenzi ambayo mara nyingi inakuwa hakuna uhalisia ni kuhisi
tuu na kuchukua hatua kali.
Mratibu wa chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) kanda ya
kaskazini, mwanasheria Happiness Mfinanga amesema jamii haipaswi kufumbia macho
ukatili ila wanapaswa kutoa taarifa kwa vyombo husika.
“Jamii ipaze sauti kwenye hilo kwani kuna vyombo vya kisheria ambavyo
vinawaelekeza kutoa ushauri ili kuepuka madhara zaidi ya ukatili majumbani
mwetu,” amesema Mfinanga.
Amesema vipo vyombo vya kutoa taarifa ikiwemo dawati la jinsia ili
kuepusha matukio ya kikatili yanayotokea kwa jamii siyo ya kufumbia macho na
ushirikiano uanze kwenye familia hadi serikalini.
Mwandishi wa habari mwandamizi Peter Saramba anasema kwa mtazamo wake,
tatizo la mwanaume kumuua mwanamke kutokana na wivu wa mapenzi ni ukatili wa
mmomonyoķo wa maadili kuanzia kwenye kuanzisha mahusiano na hata kuishi kwenye
mahusiano yenyewe.
Saramba anaeleza kuwa watu wanaingia kwenye mahusiano na hata kufikia
hatua ya ndoa bila kila mmoja kumfahamu vema mwenzake na baadhi ya walioko
kwenye mahusiano wanataka waendelee kuishi maisha yao ya mwanzo kabla ya
uhusiano.
“Jambo ambalo kiuhalisia haiwezekani kwa sababu mahusiano na ndoa ni jela
ya hiari anakoingia mtu akifahamu vema kuwa anajifunga kwa mwingine, ni kwa
sababu yeyote anayeingia jela lazima apoteze baadhi ya vitu au mambo
anayoyapenda lakini hayaruhusiwi jela,” amesema.
Amesema watu wengi waliopo kwenye mahusiano na ndoa hawazungumzi
kujadili na kutafutia ufumbuzi matatizo na changamoto zao na wanawake hutumia
silaha na mbinu za kike, hivyo hivyo wanaume kwao pia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni