Zinazobamba

Mluya: Democrasia Nchini imekua tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Na Mussa Augustine.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Democratic Party ( DP) Abdul Mluya amesema kwamba katika kipindi cha hivi sasa Democrasia imekua kwa kiwango kikubwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
Mluya amesema hayo wakati wa mahojiano na Mtandao huu ambapo amebainisha kwamba Democrasia imekua kutokana na vyama vingi vya upinzani kuongezeka huku watanzania wakiwa na uhuru wa kumchagua kiongozi wanaemtaka.

Aidha ameshauri  kuwa kinachotakiwa kwasasa ni kukamilishwa kwa mchakato wa katiba mpya ambayo ndio jambo la muhimu sana kwa vyama vya siasa hususani vyama vya upinzani.

"Swala la Democrasia mara nyingi tumekuwa tukitolea mfano nchi za dunia ya kwanza ila ifahamike kuwa tumeletewa Demokrasia ila hatujafundishwa tabia zake na jinsi ya kuishi kidemocrasia ndo maana tunalalamikia Democrasia,hivyo kwetu jambo  la msingi sana kwasasa ni kukamilisha mchakato wa katiba mpya"amesema Mluya.

Akizungumzia kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kuweka bayana atagombea nafasi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Mluya amesema kwa upande wake haoni tatizo kwani imewasaidia kumtambua mgombea wa CCM mapema ili kuweza kujiandaa namna ya kukabiliana nae.

"Kauli ya mhe rais Samia sioni kama ina shida bali  kwangu ni moja ya fursa ya kujiandaa kumpaa mgombea ambae atakuwa na sifa za kushindana nae." amesema.

Aidha Mluya amewashauri  viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, kuendelea kumshauri Rais na sio kumkosoa kwani kwa kufanya ivyo kutamsaidia kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Hakuna maoni