Zinazobamba

WAZIRI UMMY ASEMA SERIKALI YAJIPANGA NA DAWA ZISIZO NA UBORA.AZINDUA MAABARA TFDA,SOMA HAPO KUJUA

2b
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya meza kuu na wageni wa alikwa, tukio lililojiri katika viunga vya Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) leo Jijini Dar es Salaam,
 NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inazizuia na kuziondoa Vipodozi pamoja Dawa ambazo hazina ubora.
Pia Waziri Ummy ,amesema serikali hiyo imeendelea kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani kujenga viwanda vya Dawa ambavyo vitasaidia kuongezeka kwa  dawa zenye ubora.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati  akizindua maabara hamishika  zakudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema leo katika viunga vya mamlaka ya dawa, chakula na Vipodozi (TFDA).
Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata Dawa na vipodozi vyenye ubora ambavyo havina athari.

4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara hamishika hizo, wakwanza kushoto ni mwakilishi kutoka WHO Dkt. Matthius Kamwa, watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya TFDA Bi. Zainabu na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Hiiti B. Sillo.
"Serikali ya awamu ya tano inatumbua kuwa kunachangamoto ya kuwepo baadhi ya Dawa  zisizo na ubora katika jamii ambazo  huathiri  uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana na manunuzi ya  Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa kutibu mwisho hupelekea usugu wa Dawa katika mwili,na serikali hatukubali kuwepo kwa Dawa hizo"Amesema Waziri Ummy.
Amesema katika  kuhakikisha sera ya Serikali ya viwanda inatimia Wizara yake imewataka Wawekezaji wa ndani wanao taka kujenga viwanda vya dawa kuhakikisha wanakidhi  vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza kuruhusiwa kufanya shughuli hiyo ya uzalishaji wa dawa.
Aidha Mh. Ummy ameahidi kuongeza jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa  mbao ulianza 2002 unaohusu uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Maleria pamoja na Viuwa sumu.
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na kuwakamata wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri jamii na uchumi kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa dawa bandia ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017 imeshuka  kwa chini ya 1%  mafanikio haya yote yanatokana na ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na TFDA ”, amesema Sillo,  

Amesema Maabara hizo zitasambazwa sehemu mbali mbali na kudai kuwa itaweza kusaidia kuondokana na Dawa ambazo hazina ubora kwa jamii.
Amebainisha kuwa utekelezaji wa majukumu yake TFDA imepanga kupeleka maabara hizo katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo ikiwemo ofisi ya Tabora, Hospitali ya Mbeya na  Mtwara huku nyingine zitapelekwa katika vituo vya Forodha Namanga,KIA mpakani, Silali (Tarime) na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, 
1