WAZIRI WA KIKWETE AUJIA JUU UTAWALA JPM,,AIBUKA NA KUSEMA MAZITO,SOMA HAPO KUJUA
ALIYEKUWA Waziri katika serikali ya awamu ya nne ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Goodluck Ole Medeye ameibuka na kusema kwamba mazingira ya sasa ya Tanzania hayai kufanya siasa huku akimtaka Waziri wa Nishati, Merdadi Kalemani kuachia ngazi kwa kushindwa kumaliza tatizo ka kukatika umeme, anaandika Richard Makore.
Medeye amesema kwa sasa ni bora kukaa kimya nyumbani kuliko kufanya siasa kwa kuwa mazingira siyo mazuri kama ilivyokuwa awamu zingine za uongozi.
Ameyasema hayo leo asubuhi alipozungumza na Chanzo changu ameongeza kuwa kwa sasa hapa ni heri kimya kuliko kufanya siasa.
Mwanasiasa huyo ambaye alihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mwaka juzi kabla ya kuhamia Chama cha United Democratic Party (UDP), amasema bora akae nyumbani kuliko kufanya siasa.
Medeye ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba, na Maendeleo ya Makazi katika awamu ya Kikwete, amesema licha ya kuamua kukaa kimya lakini anataka, Waziri Kalemani aachie nafasi yake kwa kuwa ameshindwa kazi yake.
”Tangu juzi huku nyumbani kwangu Bahari Beach mtaa wa Kondo sina umeme kwa siku mbili, na Waziri wa Nishati yupo kwa hiyo nataka aondoke katika nafasi hiyo na kuwaachia wengine,” amesema
Tatizo la kukatika umeme limezidi kutisa nchi na jana Waziri Kalemani alitangaza kumsimamisha kazi mmoja wa maofisa wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Waziri Kalemani alisema haiwezekani nchi kuingia gizani wakati kuna watalaam ambao wanaweza kuepusha hali hiyo isitokee.
Hata hivyo, licha ya agizo hilo la Waziri na kumsimamisha kazi mtumishi huyo lakini bado mpaka sasa kuna baadhi ya maeneo hayajapata nishati ya umeme.