WAZAZI WAASWA KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI,SOMA HAPO KUJUA
WAZAZI wenye watoto walio na maradhi ya kisukari wameshauriwa kuhakikisha wanawahudumia kwa kuzingatia ushauri wa madaktari hususani katika vyakula ili maisha yao yawe salama.
Msimamizi wa Mradi wa Huduma za Kisukari kwa Watoto nchini Herieh Mganga akizungumza na waandishi wa habari.
Ushauli huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Msimamizi wa Mradi wa Huduma za Kisukari kwa Watoto nchini Herieh Mganga wakati wa zoezi la kupima wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu ili kubani kama wanaviashiria vya ugonjwa wa kisukari.
Zoezi hilo amablo limeratibiwa na Chama cha Wagonjwa wa Kisukari nchini kwa Kushirikiana na Chama cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Tamisemi lengo ni kufikia watoto wa kike katika maeneo mbali mbali nchini na kuwajengea ufahamu juu ya uwepo wa uwepo wa watoto wenye ugonjwa wa kisukari.
Amesema watu wengi wamekuwa wakifariki kwa ugonjwa huo kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kukabiliana nao.
“kwa hiyo hapa tupo tunapima urefu, uzito na mapigo ya moyo, tunapima haya ili kujua kama kunaviashiria vya ugonjwa wa kisukari na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,” amesema.
Aidha ameeleza kuwa tatizo hilo ni kubwa na kubainisha kuwa hadi sasa wamekwishaandikisha vijana Zaidi ya 2488 wenye ugonjwa huo katika kilniki 34 ambazo wanazsimamia.
Mmoja wa vijana wanachama wa Chama cha Vijana wenye kisukari nchini (TBYA) Anita Bulindi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Anita Bulindi ambaye ni mmoja wa vijana ambao ni wanachama wa Chma cha Vijana wenye Kisukari nchini (TBYA) amewataka wazazi kuamini kuwa hata watoto wanaweza kupata maradhi hayo na kuwataka wanapokutana na hali hiyo waione kama hali ya kawaida.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu jijini Dar es Salaam, Sylvia Lymo akizungumza na waandishi wa habari.
Abo
WAZAZI WAASWA KUHUSU UGONJWA WA KISUKARI,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
12:32:00
Rating: 5