Zinazobamba

NI MUNGU TU NDIYE ATAKAYEMUAKOA MSANII LULU,KESI YAKE YAFIKIA SHINGONI,SOMA HAPO KUJUA

WAZEE wa Baraza la Mahakama Kuu ya Tanzania wametoa maoni yao yanayotarajiwa kutoa tawsira ya hukumu ya kesi ya  msanii wa maigizo  Elizabeth Maichael (Lulu), anaandika Faki Sosi.
Usiku wa Tarehe 7 Aprili mwaka 2012  Lulu alidaiwa  kumuuwa bila kukusudia msanii  mwenzake, Steven Kanumba.
Baraza lenye wazee watatu wametoa maoni mbele ya Jaji,  Sam Rumanyika.
Awali kabla ya maoni ya wazee hao Jaji  Rumanyika amesoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili.
Jaji Rumanyika amesema kuwa ushahidi wa upande wa mashtaka umejikita kwenye ushahidi wa kimazingira kwa sababu Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba.
Amesema kuwa ushahidi wa kimazingira unakuwa siyo wa moja kwa moja, licha ya kuwa una vipande mithili ya nyololo ambavyo vimeshikana.
“Hivyo waungwana mkumbuke katika utoaji wa maoni yenu siyo lazima mthibitishe makosa, pia kama mkiona mshtakiwa hausiki basi msisite kuieleza mahakama,”.
Akitoa maoni yake, Mzee wa Baraza Omary Panzi amesema Lulu ameua bila kukusudia.
Amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushahidi wa mdogo wake Kanumba, Seth Bosco ambaye alielezea ugomvi uliotokea kati yake na Lulu.
“Maoni yangu ni kwamba marehemu alikufa kwa sababu ya kuteleza ikizingatiwa ilikuwa ni usiku na kulikuwa na giza, na chanzo cha kutekeleza ni ugomvi wake na Lulu,”.
Mzee wa pili, ni Sarah  amesema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi ambapo ushahidi pia umetueleza kulikuwa na giza.
” Hivyo Lulu hakuuwa makusudi bali aliuwa bila kukusudia, “.
Naye Mzee wa Tatu, Rajabu Mlawa ametoa maoni yake alisema kutokana na sababu zilizosomwa anaridhika na hakuna ubishi kuwa Lulu ana kosa la kuuwa bila kukusudia.
” Ameuwa bila kukusudia na nimeridhika na kilichosemwa, kwani Kanumba alikuwa na mwili mkubwa na alikuwa katika hali ya kulewa, hivyo inaonekana katika heka heka za ugomvi inawezekana Lulu alitumia nguvu kidogo ya kumsukuma Kanumba hadi kudondoka,”.
Baada ya  maoni hayo, Jaji Rumanyika amesema kuwa anatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo, Novemba 13 mwaka huu.