Zinazobamba

SERIKALI YAENDELEA KUWATEUA MAKADA WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO,,MSHAURI WA SHERIA WA ZITTO KABWE AULA NAFASI HII,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI Bado mambo yakiwa magumu ndani ya Chama cha Act-Wazalendo  baada ya Serikali ya Rais John Magufuli kuwateua viongozi mbali mbali wa Chama hicho na kuwapatia  kwenye serikali yake,,hali hiyo ni kama imeendelea tena baada ya Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Hallison Mwakyembe  kumteua  Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Msando ambaye ni Wakali wa Kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe anakuwa anaongozana na Makada wenzake wa Chama hicho wakiwemo,Profesa Kitila Mkumbo ambaye amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Anna Mgwhira aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ka Mujibu wa tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.
Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.
Msando ameandika  "Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya 'naomba nitoe niko vibaya'. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii".
Ameongeza "Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma"
Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.