Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AMBADILISHA KAZI ALIYEMTEUA.SOMA HAPO KUJUA

Rais Dk John Magufuli
Pia amembadilisha kituo cha kazi mkuu wa mkoa Mdeme kutoa Dodoma kwenda Ruvuma na wa Ruvuma Dk Mahenge kwenda mkoani Dodoma

Amewataka wawe wepesi wa kujibu hoja na kutatua matatizo ya wananchi ikiwamo kuleta mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo kwa wananchi.

Amesema katika utendaji wao hataki kusikia kuwa ni wageni katika nafasi zao  na kwamba wawatumikie wanyonge.

‘Zingatieni sheria na mkawatumike wanyonge, mkawe sauti yao, wasemaji wao, mtangulizeni Mungu katika utendaji wenu,’ amesema

Wakati huo huo amesema atashangazwa endapo wanafunzi vyuo vikuu wanaostahiki kupewa mikopo mwaka 2017/18 kutopata kwa wakati.

Amesema amekwisha saini bilioni 147 kwenda  wizara ya elimu  kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu wa mwaka wa kwanza wanaostahili.


“Nitashangaa sana kusikia na kuona wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo vikuu wakikosa mikopo. Nimeshasaini bilioni147 kwa ajili ya mikopo,” amesema rais Magufuli

Amemwaapisha mkuu Mkoa wa Manyara  Alexandar Pastor Mnyeti (Alikuwa DC wa Arumeru)Mkoa wa Rukwa - Mkuu wa Mkoa ni Joachim Leonard Wangabo (alikuwa DC wa Nanyumbu)

Mkoa wa Geita - Mkuu wa Mkoa ni Bwana Robert Gabriel Lughumbi (alikuwa DC wa Korogwe)

Mkoa wa Mara - Mkuu wa Mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima (aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne)

Mkoa wa Dodoma - Mkuu wa mkoa ni Bi. Christine Solomoni Mndeme (alikuwa DC wa Dodoma Mjini)
Mkuu wa Mtwara - Gelasius Gasper Byakanwa (alikuwa DC wa Hai)

Uteuzi wa Mabalozi
Dr. Aziz P. Mlima - Amekuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu wizara mambo ya nje)

IGP Mtaafu Ernest Mangu - Amekuwa Balozi
Hawa Vituo vyao vya kazi vitatangazwa

Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu wao
Ofisi ya Rais Ikulu - Katibu Mkuu Alifayo Kidata

Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na utawala Bora - Katibu Mkuu Dr. Lawrian Ndumbaro
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Dorothy Mwaluko

Ofisi ya Rais TAMISEMI - Katibu Mkuu Eng. Mussa Iyombe Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Afya) - Zainabu Chaula
Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Elimu) - Dickson Nzunda

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira - Katibu Mkuu Eng. Joseph Kizito Manongo (alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hiyo)

Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Philipo
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira - Katibu Mkuu Erick Shitindi

Bunge na Waziri Mkuu - Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi
Sera - Katibu Mkuu Faustine Kamuzora (amehamishwa kutoka ofisi ya makamu wa rais)

Wizara ya Kilimo - Katibu Mkuu Eng. Mathew Mtigumwe
Naibu Katibu MKuu - Dr. Tomas Didim Kashilila
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Mifugo - Katibu Mkuu Dr. Maria Mashingo
Uvuvi - Katibu Mkuu Dr. Yohana Budeba

Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Uchukuzi - Katibu Mkuu Dr. Leonard Chamuriho
Ujenzi - Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamuhanga
Mawasiliano - Katibu Mkuu Dr. Maria Msasabo
Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano - Eng. Adelina Madete

Wizara ya Fedha na Mipango - Katibu Mkuu Dotto James Mgosha
Naibu Katibu Mkuu Utawala - Bi. Suzan Mkapa
Naibu Katibu Mkuu Fedha za Nje - Bi. Amina Shaaban
Naibu Katibu Mkuu Sera - Dr. Hakingu M. Kazungu

Wizara ya Nishati - Katibu Mkuu Dr. Hamis Mwinyimvua (Anatoka ofisi ya Waziri Mkuu)

Wizara ya Madini - Katibu Mkuu Prof. Saimon S. Msanjila (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu)

Wizara ya Katiba na Sheria - Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome
Naibu Katibu Mkuu - Bwana Amon Mbanju

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Katibu Mkuu Prof. Adolph Mkenda (ambaye ni Mchumi, anatoka Wizara ya Biashara na Uwekezaji)
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhan Muomba Mwinyi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Katibu Mkuu Dr. Florence Nduruka
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Emmaculate Peter Ngwale

Wizara ya Mambo ya Ndani - Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rugasira
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Hassan Simba Yahaya

Wizara ya Maliasili na Utalii - katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudens Melanzi
Naibu Katibu Mkuu - Dr. Aloyce Nzuki

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Katibu Mkuu Bi. Dorothy Mwanyika (alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha)
Naibu Katibu Mkuu - Dr. Moses M. Kusiluka

Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji - Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (ametoka wizara ya habari)
Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) - Bwana Ludoviki Nduhie
Naibu Katibu Mkuu (Biashara na uwekezaji) - Prof. Joseph Bunjweshaiya

Wizara ya Elimu - Katibu Mkuu Dr. Leonard Akwelapo
Naibu Katibu Mkuu - Dr. Epifan Mdoe (anatoka Wizara Ya Madini)
Naibu Katibu Mkuu - Dr. Avie-Maria Semakaf

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Katibu Mkuu (Afya) - Dr. Mpoki Ulisubisya
Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto) - Bi. Sihaba Nkinga

Wizara ya Habari Utamaduni Usanii na Michezo - Suzan Paul Mlawi (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi)
Naibu Katibu Mkuu - Bwana Nicolaus B. William

Wiazra ya Maji na Umwagiliaji - Katibu Mkuu Prof. Kitila Mkumbo

Naibu Katibu Mkuu - Eng. Emmanuel Kalomelo