Zinazobamba

NYALANDU NI SHIDA SASA, RAIS MAGUFULI ARUSHA JIWE GIZANI KUHUSU KUHAMA KWAKE CCM,SOMA HAPO KUJUA




NA KAROLI VINSENT 
SIKU moja kupita baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye utawala wa awamu ya nne Chini ya Rais Mstaafu,Jakaya Kikwete,Lazaro Nyalandu kutangaza kukihama chama cha Mapinduzi CCM kutokana na Chama hicho kupoteza mwelekeo .
Ni wazi hatua hiyo ni kama imeleta mtikisiko ndivyo naweza kusema baada ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumrushia "Dongo"  la kiana kwa  Nyalandu 
Rais Magufuli bila kutaja jina la mtu lakini wadadisi wa mambo wanasema anamlenga Nyalandu ambaye aliwai kuwa na vyeo mbali mbali ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 
Rais Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

"Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele" alisisitiza Rais Magufuli