Zinazobamba

LAZARO NYALANDU APONGEZWA KILA KONA KWA KUHAMA CCM,ZITTO NA MSANII WEMA WANENA..LOWASSA ASEMA CHADEMA IMELAMBA DUME ,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wa awamu ya nne chini ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete,Lazaro Nyalandu   kujiuzulu nafasi ya Ubunge pamoja nafasi mbali mbali alizokuwa nazo za uongozi ndani ya CCM .kutokana na kutokubaliana na jinsi ya mambo yanavyoongozwa na Rais  John Magufuli .

Wadau mbali mbali na wachambuzi wa siasa pamoja watu maarufu wamempongeza kiongozi huyo ambaye aliwai kugombania Urais ndani ya CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015,, kwa hatua yake hiyo huku wengi wakimwita ni shujaa.

 watu hao ni pamoja Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM.

Akionyesha kuwa na furaha leo Jumatatu wakati akiongea, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.

Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.

Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani.

“Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne.

“Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kuwania urais kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa).

Lowassa alimsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.

“Nyalandu ana contacts (anafaham watu wengi) nyingi na jumuiya ya kimataifa, ni bidhaa nzuri kuwanayo,” alisema Lowassa, ambaye katika uchaguzi wa urais alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 (asilimia 39.97) ikiwa ni rekodi ya kura nyingi kwa upinzani tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992. 

 NAYE ZITTO KABWE ANENA HAYA

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amempa tano Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu kuwa ameonyesha uongozi.
Zitto ametoa maoni yake hayo baada ya Nyalandu kuamua kujiondoa CCM na kuachia nafasi yake ya ubunge.

Zitto ameandika, "Lazaro Nyalandu, umeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na kwa sababu sahihi. Kila la kheri."

Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali. 
 Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa anajisikia furaha na amani kuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa anaendelea vyema kadili siku zinavyokwenda lakini pia amegusia sakata la Nyalandu kujitoa CCM.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa anakula chakula akiwa hospitali Nairobi na kusema anajisikia vizuri kuona shujaa wao anaendelea vizuri.

"Ni jambo jema kumuona shujaa wetu anaendelea vyema kweli Mungu ni mwema siku zote, lakini pia nikiwa mkubwa nitahitaji kuwa kama Lazaro Nyalandu" aliandika Wema Sepetu
MSANII WA BONGO MUVI WEMA AFUNGUKA NAYE
Wema Sepetu ameweka ujumbe huu masaa kadhaa toka Lazaro Nyalandu alipotangaza kujivua uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuandika barua kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)