Zinazobamba

BAADA YA LAZARO NYALANDU KUJIUZULU UBUNGE CCM,WANAHARAKATI WA LHRC WAIBUKA NA NENO KALI,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
SAA chache kupita baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye utawala wa awamu ya nne chini ya serikali ya Rais mstaafu ,Jakaya Kikwete,Lazaro Nyalandu kutangaza kujizulu nafasi ya Ubunge alikuwa nayo pamoja na nafasi mbali mbali alizokuwa nazo ndani ya  Chama cha Mapinduzi (CCM),

Baada ya kusema Utawala wa Rais John Magufuli umekuwa ukikandamiza demokrasia pamoja na kuwepo matendo mbali mbali ya uvunjifu wa katiba ya nchi.

Nao, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,(LHRC) waibuka na kusema hoja anayosema Nyalandu ya ukandamizaji wa Demokrasia nchini ni ya ukweli kwani Tanzania ya sasa ipo katika kipindi kigumu cha kuminya uhuru wa kijeleza na kutoa maoni kuriko vipindi vyote.

Kituo hicho kimesema, kitendo cha Nyalandu kuhama chama ni cha haki yake  Kikatiba ila sababu ya kuhama chama anayosema ni ya msingi kutokana nchi kupitia kwenye kipindi kigumu.

Akizungumza na Mtandao huu (Fullhabari.blog) Mkurugenzii Mtendaji wa (LHRC) Dkt Hellen Kijo Bisimba amesema   kitendo cha Nyalandu kuibuka kusema hadharani ni ishara ya kuchoka na matendo hayo kutokana na  nafasi yake ya chama kutosikilizwa mpaka  kuamua kusema hadharani .
“Nyalandu anahaki kama raia ya kufanya uchambuzi,sisi kama watetezi wa haki za binadamu tunaweza kukubaliana naye kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ukandamizaji ikiwemo kutokuwepo na  haki ya kujieleza,akiwa ndani ya CCM amefanya uchambuzi ameyaona hayafai”Amesema Dkt Bisimba.

Amesema licha ya uongozi wa nyuma wa CCM kutoa uhuru wa kujieleza,kwa wananchi  huku nyuma kuwa na uhuru wa  kukosoa lakini kwa sasa hali hiyo imebadilika.

“Tumezoea miaka iliyopita uhuru ulikuwepo,lakini sahivi licha ya kuwepo kwa Haki za binadamu lakini kumekuwepo kwa sheria kandamizi ikiwemo sheria ya mtandao,leo uhuru wa Kikatiba wa kukusanyika umeminywa,Tunashuhudia Wabunge wakikamatwa”

“Kwa mfano tumeshuhudia mbunge wetu wa Kawe (Halima Mdee) amekamatwa kwa amri ya mkuu wa Wilaya na hata Rais anashindwa kumchukulia hatua Mkuu huyo wa Wilaya “Amesema Dkt Bisimba.

Hata Hivyo ,Dkt Bisimba amewataka wanajamii kutobeza uamuzi wa Nyalandu kwani ni waki yake Kikatiba.

Kujuzulu kwa Kwa Nyalandu kunakuja ikiwa ni Wiki mmoja kupita baada  Aliyekuwa Waziri wa awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete ,Goodluck Ole Medeye kusema anajitenga na Utawala wa Rais John Magufuli kwa kuwa Tanzania sio mahala pa kufanya siasa kutokana na utawala huo  unaminya  demokrasia.