Zinazobamba

TPSF YASEMA MAZINGIRA YA VIWANDA YANAHITAJI USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI

Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa 17 wa Mfuko wa Sekta Binafsi nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akikaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mfuko huo leo katika uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam
Sehemu wajumbe wa Mkutano 17 wa TPSF uliofanyika katika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam
Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF) umesema kuwa katika kujenga mazingira ya biashara kunahitaji kuwepo kwa sekta ya umma pamoja na sekta binafsi katika kuandaa maeneo tengefu ya biashara.

Hayo yamebainishwa leo Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte kwa niaba ya Mwenyekiti wa TPSF wakati akifungua mkutano wa 17 wa mwaka wa Mfuko wa Sekta ya Binafsi (TPSF) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Shamte amesema kuwa katika kuendana na mipango ya kufikia uchumi wa kati sekta binafsi na sekta ya umma zinatakiwa kushirikiana katika kuangalia mazingira ya kufanya uwekezaji wa viwanda. 

Amesema katika maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa wakuu wa mikoa , kutenga maeneo ya viwanda ambapo kuna uwezekano huo upo lakini changamoto ni miundombinu ya maeneo hayo.

Aidha ameiomba serikali kuanizisha Benki ya kuendeleza viwanda ili sekta hiyo iweze kukua na kufikia uchumi wa kati kwa kuajili watanzania wengi.

Shamte ameomba serikali kuongeza bajeti kwa mamlaka ya EPZA ili kuweza kutenga maeneo tengefu ya viwanda.


Hata hivyo amesema kuwa sekta binafsi ndio inaajiri kwa sehemu kubwa kuliko sekta ya umma, kutokana na takwimu zinaonesha kwa mwaka vijana wanahitimu 800,000 kwa sekta ya umma inaajiri vijana 40,000.