TANZANIA KUAGIZA MAFUTA LITA MILIONI 120 YA DIZELI NA MAFUTA MILIONI 80 ZA PETRORI,SOMA HAPO KUJUA
TANZANIA
inatarajia kuagiza kutoka nje ya nchi lita
Milioni 120 za mafuta ya Dizeli pamoja na lita milioni 80 za mafuta ya
Petrori ambayo yatatumika mwezi wa saba
mwaka huu.
Hayo
yameeelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Raymound Lusekelo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uigizaji mafuta kutoka nje ya
nchi wakati wakutangaza tenda kwa kampuni zitakazoshinda dhabuni ya kuingiza
mafuta hayo kutoka nje ya nchi
Lusekelo amewaambia waandishi wa habari kuwa mafuta hayo
yatarajia kuingia nchini na kusambazwa kwenye kwa wafanyabiashara wadogo wa
mafuta nchi kwa ajili ya matumizi husika.
Amesema Kampuni itakayoshinda Tenda hiyo ni ile itakayokuwa
na mitaji mkubwa pamoja na kuwepo na wataalamu wenye sifa jambo analosema
kampuni za ndani sharti ziwe na sifa hizo ili nazo ziweze kupata tenda hizo.
Hata Hivyo,Lusekelo amesema mafuta hayo yanaoingia nchini
yatakuwa ubora katika utumiaji.