TNGP MTANDANO YAWAPONGEZA WANAFUNZI WA KIKE WALIOONGOZA VYUO VIKUUU,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi habari kuhusu kuwapongeza wahitimu waliofanya vizuri katika vyuo mbalimbali nchini katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam. |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38 waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.
Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.
Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkomboa mwanamke katika changamoto mbalimbali.Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri ,
Aisha Soudy kutoka Chuo cha Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.
Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.
Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti kuliko vile wanavyofikiria.Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.