Zinazobamba

KIONGOZI WA ACT-WAZALENDO ALIYEPIGA PICHA CHAFU ,AJIUZULU UONGOZI ,SOMA HAPO KUJUA



Mkuu wa Chama Cha Act-Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa mshauri mteule wa Chama hicho Albarto Msando.

"Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo".

Zitto amesema kuwa  Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu  "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.