KIFO CHA IMAMU SALUM ,VIONGOZI WA DINI YA KIISLAM WALIANGUKIA BUNGE LA JAMHURI WA MUUNGANO,WASEMA JESHI LA POLISI LAHUSIKA NA KIFO HICHO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI Familia
ya Marehemu Imamu salum Alhamis wakiwa
wameugomea kuuzika wa Mwili marehemu huyo
mpaka pale Jeshi la polisi
litakapokubali kuhusika na kifo hicho.
Nao Shuira ya Maimamu nchini wameibuka na kulitaka
bunge la Jamhuri ya Muungani nchini kuunda tume ya kuchunguza tukio la kifo cha marehemu Salum kwa
madai kifo chake kimegubikwa na utata mkubwa.
Wamesema Maelezo ya yaliyotolewa na Kamishna wa
kanda maalum ya Polisi Dar es Salaam,Saimon Sirro kuwa Imani Salum aliuliwa na
Polisi kwa sababu ya kutaka kuiba
fedha zilizokuwa zimefikishwa kwenye mashine ya kutolea fedha
ATM maeneo ya kurasini Jijini Dar es Salaam hayaendani na maelezo ya wazazi wa
marehemu si ya kweli.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kiongozi wa Shuira ya Mamimu nchini,Sheikh
Yusuf Muhamed amesema baada ya kubaini maelezo haya ya polisi juu ya kifo hicho
hayana ukweli ndio sababu ya kulitaka bunge lichunguze ili kuondokana na
matatizo yanayotokea.
“Tunaliomba Bunge liunde kamati lichunge tukio
hili,na tume hii itakayowahusisha
wataalamu na viongozi wa kada mbali mbali,ili ichunguze kwa kina mauaji
makubwa yanayoshamiri dhidi ya raia na viongozi wa hapa nchini,”
“Ichunguzi mauaji hayo ni yale yanayifanywa na kikundi kisichoeleweka nay ale yanayofanywa
na chombo rasmi cha Dola Jeshi la Polisi”amesema Sheikh Muhamedi