KAMPUNI YA SIMU YA HALOTEL YAKANUSHA TAARIFA CHAFU JUU YAKE,SOMA HAPO KUJUA
DAR ES SALAAM: Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Mkononi ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizokuwa zinaikabili kampuni hiyo ambapo imekiri makosa yaliyotokea na kuahidi kufuata sheria za nchi katika kutoa huduma kwa wananchi.
Mashtaka yaliyokuwa yamefunguliwa yalikuwa saba lakini kampuni hiyo ilihusishwa na vipengele viwili vya mashtaka ambavyo ni kushindwa kutoa taarifa za usajili wa kampuni ya mitambo ya Unex Limited ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania nchini (TCRA) kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri ya kuuza laini za simu 1000.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Lei Van Dai alifafanua kuwa kampuni haihusiki na makosa mengine ambayo yaliwahusisha watuhumiwa wengine ambao ni wateja wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo hiyo.
Amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini kwa kufata sheria na taratibu zote za mawasiliano ambazo zinatambuliwa na TCRA.
Naye Wakili wa Kampuni hiyo, Christopher Masai alisema kwa mujibu wa mashtaka yaliyosainiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwa Mei 16, 2017 kesi hiyo ilitaja kampuni hiyo kuhusika na makosa hayo kifungu namba 6 na 7 ambavyo havihusishi kampuni hiyo na makosa ya washtakiwa wengine ambao sio wafanyakazi wa kampuni hiyo na kuongeza kwamba hawana ushirikiano wowote na kampuni hiyo pamoja na raia hao wa Pakistani zaidi ya kuiuzia laini za simu kampuni hiyo baada ya kuwasilisha nyaraka zisizo halali.
Na Denis Mtima/GPL