BODABODA BADO NI JANGA LA TAIFA,SOMA HAPO KUJUA
Moja ya ajali za bodaboda
Akitoa mikakati ya Serikali leo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kati ya mikakati hiyo ni kupitishwa kwa kanuni ya leseni ya pikipiki na bajaji pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni pamoja na vyombo vya habari.
Mhe. Mwigulu amesema kuwa mikakati mingine ni kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa waendesha bodaboda, kuimarisha usimamizi wa sheria za barabarani pamoja kusisitiza matumizi ya kofia ngumu ili kupunguza madhara pindi ajali zinapotokea.
Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa Serikali kupitia wadau mbalimbali nchini pia wanaendesha semina mbalimbali kwa waendesha bodaboda hao ili kupunguza ajali lakini pia amelitaka suala hilo lianzie kuelimishwa kuanzia ngazi ya jamii ili kulidhibiti kabisa.
Waziri Mwigulu Nchemba akijibu maswali bungeni
BODABODA BADO NI JANGA LA TAIFA,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
18:33:00
Rating: 5