MGOMO MKUBWA WA MABASI NCHINI WASITISHWA,SOMA HAPO KUJUA
: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.
Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea hatua ya kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.
Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri na Nchi Kavu (Sumatra) pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji wamekubaliana kusitisha mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo uliotakiwa kuanza kesho.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Gilliard Ngewe amesema kusitisha huko kunatokana na kikao na waziri mwenye dhamana, Profesa Makame Mbarawa juu ya kuandika kwa kutenganisha makosa ya dereva na wamiliki.
Amesema kanuni hizo zitaandikwa ndani ya siku 14 katika rasimu hiyo na wadau wa usafirishaji kuendelea usafirishaji.
Ngewe amesema kuwa baada ya kufanya marekebisho ya rasimu ya kanuni itarudishwa kwa wadau kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kupeleka bungeni.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi, Abdallah Mohamed amesema wamekubaliana na Sumatra mambo ambayo hayakuwa sawa warekebishe katika kanuni za makosa kati ya wamiliki na madereva wa mabasi.
Amesema wasipokubaliana baada ya siku 14 watarudi katika mkutano mwingine kwa kila mmoja namna gani ya kuweza kutengeneza sheria ambazo haziathiri upande mmoja.Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala , Kasmat Jaffer amesema suala ambalo limekuwa mwiba ni kosa la kufungwa pamoja na faini hali ambayo wameona ni

Reviewed by Unknown
on
19:37:00
Rating: 5