Zinazobamba

MASWALI NA MAJIBU KESI YA GAZETI LA MAWIO MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA


Maswali na majibu kati ya shihidi na wakili kibatala kesi ya uchochezi  inayomkabili Lissu na wahariri Mawio

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea na usikilizaji wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu,

Washitakiwa wengine ni pamoja na Jabir Idrissa Mwandishi mwandamizi wa gazeti la Mawio, Simon Mkina Mhariri wa gazeti la Mawio na Ismail Mahboob Meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.   

Leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Elia Athanas Rafael Hokolo aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa habari Maelezo ametoa ushahidi.

Tarehe 14 januari walilipokea nakala mbili za gazeti la mawio tolea namba 182.

Tuiona Gazeti la Mawio likiwa limebeba kichwa cha Habari 'Machafuko Yaja Zanzibar'.

Tulipeka taarifa kwa waziri kuwa ni habari yenye uchochozi ili achukue hatua.

Alidai kuwa habari hiyo ilieleza kuwa serikali ya Zanzibar inaongozwa na kufanyiwa na kufanyiwa maamuzi na Serikali ya Tanzania Bara.

Alidai kuwa kuwa habari hiyo ingeweza kuwashawishi wananchi wapinge serikali.

Alidai kuwa baada ya kupeleka taarifa hiyo kwa waziri alichukua hatua.

Amesema kuwa jambo jengine ni kuhusu mchapishaji wa gazeti hilo alikuwa hana kiapo cha kuchapisha gazeti.

Amedai kuwa kiapo kinacho fahamika hapo ni cha Morden News paper printer na sio flint Graphics.

Shahidi alisoma gazeti.

Peter Kibatala wakili upande wa utetezi alimuuliza maswali shahidi juu ya ushahidi alioutoa mahakama hiyo.

Kibatala: nilisikia ukisema kuwa moja ya majukumu yako ni kuwa msemaji wa serikali.

Shahidi: sawa.

Kibatala: kuna uhusiano gani wa kitaasisi kati ya kurugenzi ya mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo.

Shahidi: kurugenzi ya mawasiliano Ikilu ni wasemaje binafsi wa Shughuli za Rais.

Kibatala: kulingana na kuwa wateule wote wa rais hawawezi kuwa ikulu wewe boss wako ni rais.

Shahidi: ndio.

Ni sahihi kuwa unawajibika chini ya Rais

Shahidi: sahihi.

Kibatala Ni sahihi kwa ushahidi wako wewe habari hiyo ilimtaja Rais kwa jina.

Sahidi IIlimtaja.

KibatalaShahidi kwa ufahamu wako kutajwa kwa Rais na kuhusushwa na machafuko zanzibar. Ni sahihi dhana ya uchochezi unatokana na kutajwa na kuhusishwa kwa Rais

Shahidi:sawa.

kibatala: Rais alipata taarifa ya kufunguwa kwa gazeti.

Shahidi: ndio

Kibatala: Baada ya kufungiwa kwa gazeti muliwahi kupokea mrejesho wowote kutoka Ikulu.

Shahidi : hapana

Kibatala: nilikusikia kuwa wewe ulijiridhisha kuwa habari hii kuwa ni ya uchichozi pekee yako?

Shahidi: hapana tulikaa kikao .

Kibatala:Kulikuwepo kuna Ofisa yoyote wa Jeshi la Polisi kutoka kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Kuna Ofisa yoyote wa Jeshi la Polisi aliyekuja  kukuhoji.

Shahidi: ndio.

Kibatala: unankumbuka jina au cheo

Shahidi: simkumbuki.

Kibatala: unafahamu chochote kuhusu uuzwaji na usomwaji wa gazeti la Mawio kufungiwa.

Shahidi:Sijui

Kibatala: Ni sahihi kuwa kipengele cha machafuko zanzibar  hicho tu. Ndicho kilichosababisha kufungiwa kwa gazeti hilo.

Shahidi: Sahihi

Kibatala: ni sahihi kuwa gazeti la Mawio lilifunguliwa kwa amri ya mahakama ni sahihi kuwa maamuzi ya kufunga gazeti yalikuwa kinyume na sheria.

Shahidi: sijui kwa sababu nimeshastaafu kazi.

Kibatala: gazeti la MwanaHALISI liliwahi kufungwa na kufunguliwa wewe ukiwa kazini ni sahihi kuwa mulikosea.

Shahidi: kimya

Kibatala: Angalia hiyo byline (jina la Mwandishi) ya hiyo stori naonesha ni jina la nani?

Shahidi: Jabiri idrissa

Lakini huku kwenye kesi hakuna mtu anayetuhumiwa kwenye hati ya mashtaka  kuna Jabiri Idrissa Yunus

Kibatala: Nimesikia ukizungumzia suala la ripoti hiyo ni nani aliandika hiyo ripoti

Shahidi: Mimi mwenyewe

Kibatala: Kilichopelekea kuandika ripoti yako na kuona kuwa kuana viashiria vya uchochezi ni kichw cha habari au habari ya ndani?

Shahidi: Vyote

Shahidi kuna aya ya tano mwenye kuweza kuzui  machafuko haya ni Rais Magufuli kwa kumtangaza mshindi bila hivyo tutarajie umwagikaji wa damu” shahidi alinukuu.

Kibatala: Muliwahi kumuita Jabiri idirisa kabla ya kupeleka ripoti hiyo kwa ajili ya kumuhoji

Shahidi: Hapana nilimpigia simu tu.

Kibatala :Unafahamu kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliwahi kubashaniwa kisheria

Shahidi: Sijui

Kibatala: Unafahamu kuwa rais aliwahi kusikika akizungumzia matumizi ya vifaru na jeshi kwa atakayepinga uchaguzi huo.

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Wakati unafanya uchambuzi kwenye gazeti hilo ambalo uliliandika ripoti lissu alihojiwa kama Mwansiasa au Mwanasheria.

Shahidi: kimya

Kibatala: Ni sahihi kuwa Rais wa awamu iliyopita Zanzibar Abeed Amani  Karume alishindwa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais ndani ya CCM na kwamba Gharibu Bilal ndiye aliyeshinda lakini huku walimpitisha Karume

Shahidi: Sijui

Kibatala: Hayo uliyasema kuwa huyafahamu ndio uliyoyaandika kwenye ripoti uliyoipeleka kwa waziri?

Kesi hiyo itaendelea mpaka tarehe 3 Mei  mwaka 2017. ambapo shahidi ataendelea kutoa ushahidi.