Zinazobamba

MBUNGE PITER LIJUAKALI ASEMA HAYA BAADA YA KUTOA SERO,SOMA HAPO KUJUA


Mbunge wa Kilombero kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Lijualikali jana amefanikiwa kuachiwa huru na maafisa wa gereza la Ukonga baada ya kukamilisha taratibu za kutoka gerezani.

Akizungumza mara baada ya kutoka gerezani Mbunge Lijualikali aliwataka watanzania kutumia demokrasia ya kweli katika kutafuta majawabu ya matatizo waliyonayo ili kubadili taswira ya  Tanzania na kuwa nchi ya maendeleo na kuongeza mshikamano bila kubaguana.

Kwa upande wake baba mzazi wa Mbunge huyo Amberose Lijualikali aliviomba vyombo vya dola nchini kufuata sheria za nchi zinavyoelekeza katika kutoa maamuzi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani Mhe. Fredrick Sumaye aliyekuwepo katika gereza la Ukonga Dar es Salaam wakati mbunge huyo akiachiwa, aliwataka viongozi na watanzania kutumia demokrasia katika kudai haki zao ili kulinda amani ya nchi iliyopo.

Hukumu ya Lijualikali ilitenguliwa jana na Mahakama Kuu baada ya kukaa gerezani kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa masharti ya faini.