RC MAKONDA NI KIBURI,AGOMA KUJIBU TUHUMA ZA KUIBA VYETI,ASEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita
dhidi ya dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi
katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.
Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya
kufa au kupona.
“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti
na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba
tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.
Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha
na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima
zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.
“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma
bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi
ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.
Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa
ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane
moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka
ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.
Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika
ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi
imara.
Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za
kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji
la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.
“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa
za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao
wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.
Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli
ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu
Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao
haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana
walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na
vijana wachapakazi.
“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni
mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na
uhalifu,” amesema Makonda.
Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu
wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya
kuifanya Kigamboni tulivu na salama.
Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya
watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia
vijana kuchungana wao wenyewe.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la
tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha
vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya
mazoezi.
Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo
hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo